Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, August 13, 2013

Meneja matukio TBL kanda ya nyanda za juu kusini Godfrey Mwangungulu asherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Nuru uyole Mbeya

 Meneja matukio TBL kanda ya nyanda za juu kusini Godfrey Mwangungulu akimkabidhi zawadi zenye dhamani ya shilingi laki tano kwa  mlezi wa watoto hao Bi Dorris Silavwe


Watoto wakifurahia zawadi walizopewa na Mwangungulu wakibeba kwa kusaidiana kupeleka ndani

 Meneja matukio TBL kanda ya nyanda za juu kusini Godfrey Mwangungulu akiwagawia pipi watoto wakituo hicho


Mlezi watoto hao katika kituo hicho, Dorris Silvwe amemshukuru Mwangungulu  kwa kuonyesha upendo na kuwajali watoto hao na amemwomba asichoke kuwatembelea mara kwa mara watoto hao kujua wanaendeleaje


Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo Bw Geofrey Mwangungulu alisema kuwa amelazimika kutoa zawadi hizo   ili kusherehekea nao katika siku yake ya kuzaliwa  kama njia ya kuwajali.

Hata hivyo alitaka jamii kuendelea kuwakumbuka watoto hao yatima badala ya kuendelea kuwatenga na kuwanyanyapaa kwa madai kuwa watoto hao yatima hawakupenda kuwa yatima ila ni mipango ya Mungu na kuwa jamii kuendelea kuwabagua ni kuongeza unyanyapaa kwa watoto hao wasio na hatia mbele za Mungu.1 comment: