Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, August 30, 2013

MKUU WA MKOA WA MBEYA, ABBAS KANDORO ALICHARUKIA JIJI LA MBEYA KWA UCHAFU WA MAZINGIRA.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amelazimika kuingilia kati kunusuru hali ya uchafu iliyokithiri ndani ya jiji la Mbeya kwa kuwataka Viongozi kusimamia Sheria.

Mkuu wa wilaya Mbeya Norman Sigalla akimkaribisha mkuu wa mkoa Mbeya kuongea na wadau wa jiji la Mbeya

Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga akielezea jinsi walivyojipanga kuanza kazi ya kuliweka jiji kuwa safi

Mkurugeni wa jiji la Mbeya Musa Zungiza

Wadau mbali mbali wa jiji la Mbeya wakimsikiliza mkuu wa mkoa Mbeya





 JIJI LA MBEYA LAJIPANGA KUHAKIKISHA USAFI WA MAZINGIRA UNAIMARISHWA.

ATAKAYEKAMATWA KUTUPA UCHAFU OVYO KULIPA FAINI 50,000/=.

 ATAKAYEMKAMATA NA KUMPELEKA MTUPA TAKA OVYO ATAPEWA 20,000/= PAPO HAPO.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amelazimika kuingilia kati kunusuru hali ya uchafu iliyokithiri ndani ya jiji la Mbeya kwa kuwataka Viongozi kusimamia Sheria.

Kandoro amesema Jiji la Mbeya ndiyo taswira ya Mkoa mzima hivyo hali ya uchafu inapozidi inatoa picha ya Mkoa mzima ambao utaonekana kuwa na sifa ya uchafu.

Amesema Jiji la Mwanza linaloongoza kwa Usafi kila Mwaka lina watu na wananchi kama wanaoishi Mkoani Mbeya husasani katikati ya Jiji la Mbeya na kushangazwa na kitendo cha kutopenda hali ya usafi.

Kutokana na hali hiyo Kandoro ameagiza viongozi wa Serikali za Mitaa, Kata na Halmashauri ya Jiji kuhakikisha wanasimamia na kutekeleza sheria ya Usafi wa mazingira na matokeo yake yapatikane ndani ya mwezi mmoja.

Hivyo sheria ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya inasema atakayebainika kutupa takataka sehemu isiyoruhusiwa atalipa faini ya Shilingi 50,000/= huku mtu yeyote atakayemkamata anayetupa taka na kumfikisha kunakotakiwa atalipwa 20,000 papo hapo.

Hayo yamebainishwa katika mkutano wa Wadau wa Usafi wa Mazingira ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro uliofanyika katika ukumbi wa Mkapa Sokomatola Jijini Mbeya.

Kutokana na maagizo hayo baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo wameunga mkono suala hilo na kwamba ajira zitaongezeka kwa vijana kuwawinda wanaochafua mazingira na kujiongezea kipato.

Na mbeya yetu

1 comment:

Anonymous said...

Napenda mkakati uliwekwa kwa ajili ya kulifanya jiji kuwa safi, swali langu ni je? tutawakamata vipi? watupaji taka wa soko dogo la Magorofani ambao wanatupa takataka zao karibu na kituo cha Polisi, karibia zinaziba barabara.
By mwana mazingira.