Picha ya pamoja
MFUMO
mpya wa utekelezaji wa Mfuko wa maendeleo ya jamii(TASAF) wa awamu ya tatu wa
mpango wa kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi nchini,
umepokelewa kwa mwitikio mkubwa na wadau wa maendeleo wilayani hapa.
Aidha
baadhi ya wadau hao pia wameipongeza Serikali ya awamu ya nne kwa kutengeneza
miradi ambayo humnufaisha mwananchi moja kwa moja kwa kupitia wawakilishi wao
ambao ndiyo wanaotakiwa kuchagua na kupendekeza miradi ya kutekelezwa.
Hayo
yalibainshwa wakati wa Washa ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara na
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya kuhusu mradi wa
awamu ya tatu wa Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) iliyofanyika katika ukumbi
wa Mamlaka ya maji uliopo katika mji mdogo wa Rujewa Wilayani hapa.
Walisema
mpango wa kunusuru kaya maskini ni mzuri kutokana na kuwalena wananchi moja kwa
moja katika ngazi za vijiji na mitaa wanayoishi baada ya kukidhi vgezo
vitakavyokuwa vimewekwa na TASAF pamoja na uwezeshwaji uliotolewa kwa Madiwani
ambao ni wawakilishi wa wananchi.
Akizungumza
kwa niaba ya Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Kenneth
Ndingo alisema utekelezaji wa mradi wa awamu ya tatu utafanikiwa zaidi tofauti
na miradi iliyopita kutokana na wahusika kufika jirani na maeneo ambayo miradi
itatekelezwa.
Aliongeza
kuwa mpango wa kupunguza umaskini ni mzuri na utaleta manufaa makubwa kwa
maendeleo ya nchi baada ya wananchi wa hali za chini kuwezeshwa kiuchumi baada
ya kupatiwa misaada na kufundishwa namna ya kujishughulisha na ujasiliamali.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbarali, Mhandisi Venant
Komba Mradi wa awamu ya Tatu utafanikiwa endapo changamoto zilizoonekana
katika awamu ya pili zitaondolewa mapema kabla ya mradi kuanza.
Alizitaja
baadhi ya changamoto zilizojitokeza katika awamu ya pili kuwa ni pamoja na
gharama kubwa za kuendeshea miradi kuwa tofauti na fedha halali zinazotolewa na
Tasaf hivyo kuzifanya Halmashauri kutafuta fedha kutoka katika vyanzo vingine
vya mapato.
Alisema
changamoto nyingine ilikuwa ni elimu kwa wananchi ambao ndiyo walengwa wakubwa
kutokuwa na mwitikio wa kuchangia baadhi ya michango ambayo walipaswa kuchangia
kama mradi ulivyokuwa umeainishwa.
Alisema
katika awamu ya pili jumla ya miradi 87 katika Kata 10 na vijiji 50
ilitekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.5 ambapo wananchi
walichangia shilingi Milion 234,797, 450 katika kufanikisha miradi hiyo ambayo
imekamilika yote kwa asilimia mia moja isipokuwa mradi mmoja ambao fedha zake
zilichelewa kufika.
Naye
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Taifa, Mhandisi Elisifa
Kinasha,ambaye pia ni Meneja miradi wa Mfuko huo alisema mpango wa awamu ya
tatu umelenga kunusuru kaya maskini kutokana na athari za umaskini na
kuziwezesha kupata mahitaji ya msingi, kulinda rasilimali zao na kuwekeza kwa
maendeleo yao.
Alisema
mradi huo umegawanywa katika sehemu kuu nne ambao utatekelezwa kwa kipindi cha
miaka 10 kwa awamu ya miaka mitano mitano ambapo alizitaja sehemu hizo kuwa ni
pamoja na Kunusuru kaya maskini na zilizo katika mazingira hatarishi.
Sehemu
nyingine ni kuinua hali ya maisha na kuongeza kipato kwa kutoa msaada kwa watu
wenye kuonyesha jitihada katika kuboresha kipato na kuinua hali za maisha kwa
kuweka akiba.
Alisema
sehemu nyingine itakuwa ni ujenzi wa miundombinu katika vijiji ambavyo havina
miundombinu au huduma kuwa mbali ili kuwasaidia walengwa kuweza kutimiza
masharti ya mpango huo.
Alesma
sehemu ya mwisho ya mradi huo itakuwa ni kujenga uwezo kwa kutoa mafunzo kwa
wadau katika ngazi zote za taifa, Mkoa, Wilaya, Kata, Vijiji na Shehia ambapo
mafunzo yatatolewa ili utekelezaji wa mpango ufanyike kwa mujibu wa utaratibu
na hivyo kufanikisha malengo yaliyowekwa.
Mhandisi
Kinasha aliongeza kuwa katika mradi wa awamu ya tatu jumla ya kaya 275000
zitanufaika kwa nchi nzima ambapo kwa kuanzia mradi utaanza katika Halmashauri
14 ikiwemo Wilaya ya Mbarali iliyoteuliwa katika Mikoa ya Rukwa na Mbeya
kutokana na utafiti uliyofanyika mwaka 2011.
Aidha
katika Washa hiyo ilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Gulam Hussein
Kiffu kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro, ambapo alisema mradi
huu ili ufanikiwe ni lazima ushirikishwaji wa wadau uzingatiwe.
Aliongeza
kuwa mradi huu ulizinduliwa na Raisi Kikwete Agosti 15, mwaka jana Mkoani
Dodoma baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa awamu ya kwanza na awamu ya pili.
Alisema
wadau waliopatiwa mafunzi ni vema wakatekeleze kile walichofundishwa kwa
kuwafikia walengwa na kutoa elimu kuhusu mradi huo ili isiwe na vikwazo wakati
wa utekelezaji wake.
Hata
hivyo Washa hiyo itafanyika kwa siku tano kwa kuwajengea uwezo Madiwani, Wakuu
wa Idara na wataalamu wa Halmashauri ili kuwawezesha kutoa elimu kwa wananchi
ambao watafikiwa na mradi ili kurahisisha utekelezaji wake.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment