Mlezi watoto hao katika kituo
hicho, Dorris Silvwe amemshukuru Mwangungulu kwa kuonyesha upendo na kuwajali watoto hao na amemwomba asichoke
kuwatembelea mara kwa mara watoto hao kujua wanaendeleaje
Akizungumza
baada ya kukabidhi msaada huo Bw Geofrey Mwangungulu alisema kuwa amelazimika
kutoa zawadi hizo ili kusherehekea nao katika siku yake ya kuzaliwa kama njia ya kuwajali.
Hata hivyo alitaka jamii kuendelea kuwakumbuka
watoto hao yatima badala ya kuendelea kuwatenga na kuwanyanyapaa kwa madai kuwa
watoto hao yatima hawakupenda kuwa yatima ila ni mipango ya Mungu na kuwa jamii
kuendelea kuwabagua ni kuongeza unyanyapaa kwa watoto hao wasio na hatia mbele
za Mungu.
|
1 comment:
Safi sana hiyoooo!
Post a Comment