Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, August 27, 2013

MBUNGE WA JIMBO LA RUNGWE MAGHARIBI, PROFESA DAVID MWAKYUSA ACHANGISHA ZAIDI YA MILIONI 40 KWA AJILI YA UJENZI WA KANISA LA SABATO LA SWEBO- NTOKELA WILAYANI RUNGWE.

Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa akizungumza na waumini wa kanisa la Wasabato wa Swebo Ntokela kuashiria ufunguzi wa harambee ya ujenzi wa kanisa.

Watoto wakiingia kanisani kwa ukakamavu mkubwa kushiriki harambee hiyo.
Mgeni rasmi Profesa Mwakyusa akiwa meza kuu pamoja na viongozi wa Kanisa la Sabato siku ya harambee.
Kwaya ya Kanisa hilo ikitumbuiza kanisa hapo siku hiyo ya harambee.
Katibu mkuu wa kanisa la Sabato Jimbo la Nyanda za juu kusini Mchungaji Steven Letter akisoma neno la Mungu kuashiria ufunguzi wa Harambee hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa na waumini wakifuatilia kwa makini zoezi la Harambee lililokuwa likiendelea kanisani hapo.
Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Harambee hiyo, Award Mpandilah  na Jose Mwapamba wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi.
Award Mpandila akisimamia zoezi la uchangiaji wa harambee lilipokuwa likiendelea.
Kamati ya maandalizi ya harambee hiyo ikiwa katika picha ya pamoja.
Award Mpandila akimkabidhi hesabu ya jumla ya fedha zilizopatikana katika harambee hiyo Mgeni rasmi Profesa Mwakyusa.
Mwonekano wa jengo la kanisa hilo lilipoishia na kulazimu kufanya harambee ili kumalizia ujenzi wake.


Profesa David Mwakyusa Waziri wa Afya wa Zamani  na Mbunge wa sasa wa Jimbo la Rungwe Magharibi(CCM) amefanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Milion 40 katika harambee ya uchangiaji ujenzi wa kanisa la Sabato la Swebo lililopo Ntokela Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Katika Harambee hiyo  Profesa Mwakyusa ambaye alikuwa Mgeni rasmi, kabla ya kuanza kwa zoezi hilo aliwasihi waumini  wa kanisa hilo kuacha tabia ya kunung’unika pale wanapojitoa kwa ajili ya kusaidia shughuli mbali mbali za kikanisa ambazo zinafanywa na makanisa hayo  ili kusaidia jamii.

Imeelezwa kuwa baadhi ya waumini wamekuwa na moyo wa kujitolea pindi misaada mbali mbali inapohitajika katika makanisa, badala yake huanza kuumia  katika mioyo yao kwa kile walichotoa kwa kuona wametoa kiasi kingi.

Prof. Mwakyusa alisema  kama waumini wameamua kujitoa kwa ajili ya shughuli  za kanisa  hawana budi kunung’unika ndani ya nafsi zao kwani kazi ya mungu ni kujitolea si busara muumini kutoa msaada halafu ujutie baadaye.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi  mmoja wa wajumbe wa kamati  ya maandalizi  ya harambee hiyo  Bw.Awadi Mpandila  alisema kuwa lengo la kuanzisha ujenzi huo wa kanisa kulitokana na wingi wa waumini katika  kanisa hilo ambao wanafikia 835.

Award alisema kuwa ujenzi huo ulianza  mwaka 2002 na kiasi cha fedha kilichotumika mpaka sasa ni mil.279 na zinazohitajika ili kuweza kukamilisha jengo
hilo ni sh. Mil.90.

Mbali na kukamilika kwa Harambee hiyo Mpandila anatoa wito kwa wadau na marafiki wa karibu ambao walipewa kadi za mwaliko lakini walikwama kufika kuendelea kuchangia kutokana na fedha zilizopatikana kutokidhi kiwango.

Alisema fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kupaua na kumalizia jengo la kanisa hilo ambalo hatua za ujenzi wa awali umekamilika hivyo Wadau na marafiki wamekumbushwa kumtolea Mungu kupitia ujenzi wa kanisa hilo.

Hata hivyo katika harambee hiyo jumla ya sh. Mil.46 zilipatikana huku fedha iliyochangwa papo kwa papo ni sh. Mil.23 huku ahadi zikiwa mil.23 .

Aidha katika harambee hiyo ,Prof. Mwakyusa alichangia zaidi ya mil.2 pamoja na familia yake.

Na Mbeya yetu

No comments: