Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, August 26, 2013

MASHINDANO YA NETIBOLI KLABU BINGWA LIGI DARAJA LA KWANZA TAIFA YAANZA MBEYA JUMLA YA TIMU

Mkuu wa wilaya Mbeya  Norman Sigalla akifungua mashindano ya klabu bingwa ligi kuu mpira wa mikono daraja la kwanza Taifa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
 Mwenyekiti wa Chaneta tanzania, Annie Kibira, alisema kuwa  jumla ya 12 ndizo zinazoshiriki michuano hiyo na kwamba michuano hiyo ikakuwa ikizechezwa kila asabuhi na Jioni hadi siku ya fainali.
Katibu mkuu CHANETA  Maimuna Mrisha akimshukuru mgeni rasmi mara tu baada ya ufunguzi wa michezo hiyo
Mkuu wa wilaya Mbeya  Norman Sigalla akisalimiana na timu ya Hamambe kabla ya kupambana na timu ya FBF toka DSM
Hamambe wakipambana na FBF toka Dsm
Mbeya. Wenyeji wa mashindano ya mpira wa netiboli, yanayofanyika kitaifa Mkoani Mbeya, timu ya Hamambe na Polisi za Jijini Mbeya zimeanza vibaya katika michuano yao uliochezwa juzi baada ya kukubali kipigo na timu ya Filbert bay foundationa (FBF) ya pwani na Polisi Arusha.

Michuano hiyo inafanyikia katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya, ambapo katika  mechi za ufunguzi wa mashindino hayo jumla ya timu sita zilichuana vikali huku timu ya Hamambe inayomilikiwa na halmashauri ya Jiji la Mbeya ilifunguwa na timu ya Fbf ya pwani jumla ya mabao 36-26, huku Polisi Mbeya nayo iliyocheza na Polisi Arusha ilifungwa mabao  20-18.

Timu zingine zilizocheza ni pamoja na Jeshi Star kutoka Dar Es salaam iliyocheza na Jkt Ruvu ya Pwani ambapo    Jeshi star iliifunga Jkt Ruvu mabao 21-14, huku timu ya Ttpl kutoka Morogoro ilifanikiwa kuibamiza timu ya CMTU ya Jijini Dar es Salaamu jumla ya mabao 30-15.

Hata hivyo mtetezi wa kombe hilo Timu ya Fbf inaonekana kufanya  vizuri katika mechi zote ambazo zimekwisha kucheza uwanjani hapo na kwamba huenda  ikafanikiwa kuchukuwa tena ubingwa wa ligi hiyo.

Aidha, timu nyingine ni pamoja Magereza kutoka Morogoro iliifunga timu ya Polisi Mwanza jumla ya mabao 38- 20 na timu ya Jkt Mbweni  ilifanikiwa kuifunga timu ya Uhamiaji zote za Jijini Dar es Salaamu  mabao 35-17.

 Mwenyekiti wa Chaneta tanzania, Annie Kibira, alisema kuwa  jumla ya 12 ndizo zinazoshiriki michuano hiyo na kwamba michuano hiyo ikakuwa ikizechezwa kila asabuhi na Jioni hadi siku ya fainali.

Na Mbeya yetu

No comments: