Mbeya. Wenyeji wa
mashindano ya mpira wa netiboli, yanayofanyika kitaifa Mkoani Mbeya, timu ya
Hamambe na Polisi za Jijini Mbeya zimeanza vibaya katika michuano yao
uliochezwa juzi baada ya kukubali kipigo na timu ya Filbert bay foundationa
(FBF) ya pwani na Polisi Arusha.
Michuano hiyo inafanyikia
katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya, ambapo katika mechi
za ufunguzi wa mashindino hayo jumla ya timu sita zilichuana vikali huku timu
ya Hamambe inayomilikiwa na halmashauri ya Jiji la Mbeya ilifunguwa na timu ya
Fbf ya pwani jumla ya mabao 36-26, huku Polisi Mbeya nayo iliyocheza na Polisi
Arusha ilifungwa mabao 20-18.
Timu zingine zilizocheza
ni pamoja na Jeshi Star kutoka Dar Es salaam iliyocheza na Jkt Ruvu ya Pwani
ambapo Jeshi star iliifunga Jkt Ruvu mabao 21-14, huku timu
ya Ttpl kutoka Morogoro ilifanikiwa kuibamiza timu ya CMTU ya Jijini Dar es
Salaamu jumla ya mabao 30-15.
Hata hivyo mtetezi wa
kombe hilo Timu ya Fbf inaonekana kufanya vizuri katika mechi zote
ambazo zimekwisha kucheza uwanjani hapo na kwamba huenda ikafanikiwa
kuchukuwa tena ubingwa wa ligi hiyo.
Aidha, timu nyingine ni
pamoja Magereza kutoka Morogoro iliifunga timu ya Polisi Mwanza jumla ya mabao
38- 20 na timu ya Jkt Mbweni ilifanikiwa kuifunga timu ya Uhamiaji zote
za Jijini Dar es Salaamu mabao 35-17.
Mwenyekiti wa Chaneta tanzania, Annie Kibira, alisema kuwa
jumla ya 12 ndizo zinazoshiriki michuano hiyo na kwamba michuano hiyo
ikakuwa ikizechezwa kila asabuhi na Jioni hadi siku ya fainali.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment