Watu mbalimbali wakiwa katiaka viwanja vya Mwakangale Nane nane kwa ajili ya Kumsikiliza Mgeni Rasmi
Ebony FM Radio wakiwa LIVE viwanja vya Nanenane
Kikundi cha TOT Mbeya wakitumbuiza katika Shughuli za uzinduzi wa Nanenane Mbeya
Mgeni Rasmi Waziri wa Uchukuzi Dr. Halison Mwakyembe Katikati akiwa meza kuu pamoja na viongozi mbalimbali
Viongozi mbalimbali wakiwa katika Meza kuu
Katibu wa TASO Kanda ya nyanda za Juu Kusini Ramadhani Kiboko akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi
Waziri wa Uchukuzi ambaye alikuwa mgeni Rasmi Dr. Harison Mwakyembe akihutubuia.Waziri wa
Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ametoa miezi mitatu kwa matrekta yote
yanayobeba makontena Bandarini kuondolewa na kupelekwa kwa wakulima mashambani kwa ajili ya
shughuli za kilimo huku akisisitiza kwamba kazi hiyo siyo mahali pake.
Kauli hiyo ameitoa
leo kwenye ufunguzi wa maonyesho ya kilimo ya wakulima ya nane
nane ambayo kwa nyanda za juu kusini yanayofanyika Jijini Mbeya katika
viwanja vya John Mwakangale Vilivyopo Uyole ambapo kauli mbiu
yake ikiwa ni “Zalisha Mazao ya Kilimo na Mifugo kwa kulenga Mahitaji ya Soko”.
Amesema ifikapo Octoba
30 mwaka huu matrekta yote yawe yameshaondolewa ambapo pia atawasiliana na
jeshi la Polisi pamoja na Sumatra kuhakikisha wanasimamia
zoezi hilo.
Amesema Matrekta mengi ameyaona bandarini yakitumika
kubeba mizigo, kwa mfano makontena, hivyo ameyataka matrekta hayo yanayotumika
bandarini yaende yanakohitajika kwenye kilimo hivyo hataki s kuyaona
bandarini.
Amesema Serikali
imeweza kufuta ushuru wa zana za kilimo kama matrekta chini
ya kampeni ya Kilimo Kwanza, lakini matrekta mengi yaliyoingizwanchini ili kuwezesha kilimo
kukua yameishia kubeba mizigo bandarini kitu ambacho Serikali haiwezi kukubali
kuona yanatumika kwa kazi hiyo.
Amesema uzalishaji wa
mazao ya kilimo na mifugo katika mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ipo
chini ikilinganishwa na viwango vya utafiti, mfano hekta moja ya zao la mahindi
inazalisha wastani wa tani tatu lakini utafiti unaonesha kwamba hekta moja ya
zao la mahindi inaweza kuzalisha wastani wa tani saba za mahindi.
Aidha akizungumzia kwa
upande wa maziwa wastani wa uzalishaji kwa ng’ombe mmoja kwa siku ni lita saba
wakati kiwango kinachotakiwa kuzalishwa ni lita 20 kwa ng’ombe kwa siku.
Dk. Mwakyembe amesema upo umuhimu
mkubwa wa kuyaongezea thamani mazao kwa njia ya viwanda vidogovidogo ili
yauzike kwa haraka na kwa bei nzuri zaidi na kukidhi matakwa mbalimbali ya
soko.
Ameongeza kuwa mikoa ya
Nyanda za Juu Kusini imetengewa zaidi ya Shs. 5 bilioni kwa
kazi ya kukarabati barabara vijijini, matumizi ya fedha hizo yakisimamiwa
vizuri itasaidia kuleta mabadiliko katika kusafirisha mazao vijijini.
Kuhusu sekta ya uchukuzi
wa anga, reli na majini,alisema serikai inaendelea kuimarisha reli ya TAZARA
kwa ushirikiano wa Serikali zetu mbili za Tanzania na Zambia, tuko kwenye
maandalizi ya ujenzi wa reli kutoka Uyole kwenda Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira,
kuunganisha Tunduma na bandari ya Kasanga katika Ziwa Tanganyika.
***
Picha zote na Mbeya Yetu Blog
No comments:
Post a Comment