Amir-Jamaat
Ahmadiyya Tanzania, Tahir Mahmood Chaudhry
Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Mkoa wa Mbeya itafanya mkutano wenye
lengo la kuzungumzia mchango wa dini katika kuleta amani ya taifa na dunia kwa
ujumla.
Mkutano huo utafanyika siku ya Jumanne tarehe 20/08/2013 katika ukumbi
wa mikutano wa Benjamin Mkapa kuanzia saa kumi Alasiri. Inshallah.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
mkutano huo. Aidha viongozi na watendaji kadhaa wa serikali katika ngazi
mbalimbali mkoani Mbeya pamoja na viongozi wa Jumuiya za kidini na asasi sisizo
za kiserikali wamealikwa kwenye mkutano huo, na baadhi yao watapata nafasi ya
kuzungumza katika mada hiyo muhimu.
Jumuiya ya Waisamu Waahmadiyya inauona mkutano wa aina hii kuwa ni
muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho taifa letu linapita katika wakati mgumu
wa mivutano baina ya wanadini wenyewe kwa wenyewe na wakati mwingine na
serikali.
Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya ambayo ni Jumuiya ya kimataifa
ilianzishwa na Seyyidna Mirza Ghulam Ahmad a.s. katika kijiji cha Qadiani India
mnamo mwaka 1889 kufuatia wahyi alioupokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba
amemtuma ili kuwa Masihi na Imam Mahdi wa zama zetu. Hapa nchini Jumuiya ya
Ahmadiyya ilisajiliwa rasmi mwaka 1934.
Tangu kusajiliwa kwake pamoja na kujihusiaha na masuala ya kueneza dini
ya Kiislam kwa amani, Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya imesaidia kukuza Lugha ya
Taifa kwa kutoa tafsiri ya kwanza ya Qu’ran Tukufu kwa Kiswahili mwaka 1953.
Jumuiya pia inajihusisha na utoaji wa hudum aza kijamii na misaada ya
kibinadamu kila inapowezekana hasa kupitia shirika lake la Kimataifa Humanity
First. Jumuiya imeweza kusaidia katika ukarabati wa visima vya maji safi
vipayavyo 50 kwenye maeneo mbalimbali nchini katika kipindi cha miaka miwili
iliyopita. Pia misaada ya vifaa vya maabara, kompyuta, mabegi ya shule, kalamu
na madaftari ya kuandikia yametolewa kwenye shule kadhaa nchini yakilenga zaidi
maeneo ya wanaohitaji. Kwa sasa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya duniani
inaongozwa na Khalifa wa Tano wa Masihi aliyeahidi Hadhrat Mirza Masroor Ahmad
a.t.b.a. huku ikiwa na matawi yake katika nchi 202 duniani.
Wassalaam;
________________
Tahir Mahmood Chaudhry
AMIR – JAMAAT AHMADIYYA TANZANIA.
1 comment:
Ukweli Mbeya yetu nawakubali sababu ya kupost habari bila kuchangua dini inanifanya niwe mdau mkubwa wa blog yenu
Post a Comment