Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, July 4, 2013

MUAFAKA WA KUPATA MKOA MPYA WAPATIKANA SASA KUITWA SONGWE


  MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO AKIFUNGUA MKUTANO WA KAMATI YA USHAURI YA MKOA(RCC)  JIJINI MBEYA
 KATIBU TAWALA WA MKOA MARIAM MUTUNGUJA AKISOMA TAARIFA YA MKUTANO
 NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI PHILIPO MULUGO AKICHANGIA JAMBO WAKATI WA KIKAO HICHO
 MBUNGE WA MBOZI MASHARIKI NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MBEYA GODFREY ZAMBI AKICHANGIA JAMBO KATIKA KIKAO HICHO
 MKUU WA WILAYA WA MBEYA  DR. NORMAN SIGARA  AKIZUNGUMZA  KATIKA MKUTANO HUO
 MBUNGE WA VITI MAALUMU(CCM) MKOA WA MBEYA  DR. MARY  MWANJELWA  AKICHANGIA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO.
 MEYA WA JIJI MBEYA ATANAS kAPUNGA AKICHANGIA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO
 MKUU WA  WILAYA YA  RUNGWE  CRISPIN MEELA AKIZUNGUMZA JAMBO WAJUMBE  WAKIWA WANAFUATILIA MKUTANO HUO
 
Songwe ndilo jina lililopendekezwa kuitwa kwa Mkoa Mpya utakao gawanywa kutoka Mkoa wa Mbeya ambao utakuwa na Wilaya za Ileje, Chunya, Mbozi na Momba ambapo Makao makuu ya Mkoa huo utakuwa Mkwajuni Wilayani Chunya.

Mkoa wa zamani Mkoa wa Mbeya utabaki na Wilaya za Rungwe, Mbarali, Mbeya na Kyela ambapo Makao makuu yatabaki pale pale Jijini Mbeya.

Kupatikana kwa jina hilo na mwafaka huo umetokana na Mkutano wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa uliofanyika leo katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.

Jina la Mkoa huo Mpya limetokana na uwepo wa Uwanja wa Ndege wa Songwe na Mto mkubwa unaoitwa Songwe ambao umezipitia Wilaya zote zinazounda Mkoa huo mpya.

Hata hivyo kuhalalishwa kwa jina na Mkoa huo unategemewa na Mamuzi ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete baada ya kupelekewa mapendekezo hayo ya RCC.
 
PICHA, HABARI  NA MBEYA YETU 

1 comment:

Anonymous said...

Mkwajuni! Panahitaji nguvu ya ziada kupafanya makao makuu ya mkoa achilia mbali wilaya; hizo fedha mtazitoa wapi na je ni muhimu kweli?