Wakala Mkuu wa Usambazaji wa mbegu za Highland Seed Growers, Tito Tweve.
Wakala wa Usambazaji wa mbegu za Highland Seed Growers, Award Mpandile akizungumza jambo na wakulima wa Mahindi kuhusu uzuri wa mbegu hizo vijijini.
Meneja Masoko wa Kampuni ya kuzalisha mbegu ya Highland Seed Growers John Mbele akitoa elimu kwa Wakulima wa kata ya Ikuwo jinsi mbegu hizo zinavyostahimili hali ya hewa na mahitaji ya watanzania.
Wakulima wa Kata ya Ikuwo wakifuatilia kwa makini elimu juu ya Mbegu ya Mahindi iliyofanyiwa utafiti na Chuo cha Kilimo cha Uyole aina ya UH 615.
Diwani wa Viti Maalum kata ya Ikuwo Tuli Mwasanga akigawa mbegu kwa Wakulima
Mkulima akitoa maoni yake kuhusu mbegu hizo
Afisa Masoko akiwa katika picha ya pamoja aada ya kumaliza mkutano
Wakulima wakigawiwa mbegu kwa ajili ya majaribio
Meneja Mauzo na Wakala wa mbegu wakiangalia shamba la mfano lilivyozalisha vizuri
Afisa kilimo wa kata ya Ikuwo Olimpa Ukwama akizungumza jambo
Diwani wa Kata hiyo Antony Sanga
Baadhi ya Maafisa Kilimo wakitoa somo
Wakulima wakisikiliza kwa Makini .
Picha na Mbeya Yetu
********
Katika kuhakikisha Sera ya
Serikali ya Kilimo kwanza inafanikiwa kwa Vitendo, Kampuni ya Kusambaza Mbegu
Mbali mbali zinazofanyiwa utafiti na Chuo cha Kilimo cha Uyole Jijini Mbeya
imeanza kuwasambazia Wakulima wa Vijijini mbegu bora za Mahindi aina ya UH 615.
Neema hiyo imeanza kuwanufaisha
Wakulima wa Wilaya za Makete Mkoani Njombe, Rungwe na Halmashauri ya Jiji la
Mbeya Mkoani Mbeya baada ya Kampuni hiyo kusambaza mbegu ambazo wakulima
wamezisifu kuwa zinazalisha mazao mengi tofauti na mbegu zingine.
Akizungumza na Wakulima wa
Kijiji cha Ikuwo Wilayani Makete katika Mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya kujua jinsi wakulima wanavyokumbana na
changamoto za Mbegu hizo mpya Wakala wa Usambazaji wa Mbegu za Highland Growers
Ltd, Award Mpandile amesema lengo la kutengenezewa mbegu hizo ni kukabiliana na
hali halisi ya hali ya Hewa ya asili ya Mtanzania.
Amesema Mbegu nyingi
zinazolimwa na Wakulima haziwasaidii kutokana na kutoa Pumba nyingi badala ya
Unga pamoja na kushindwa kustahimili magonjwa mbali mbali hali inayopelekea
Wananchi wengi kushindwa kupata maendeleo.
Kwa upande wake Meneja Masoko
wa Kampuni hiyo, John Mbele amesema ni
kampuni chache zinazotengeneza bidhaa na kuwauzia watumiaji lakini baadaye
wakaenda kuwauliza wananchi namna wanavyoipokea na matunda yake pamoja na
changamoto.
Baadhi ya Wakulima wa Kijiji
cha Ikuwo wamesema mbegu zilizoletwa na Kampuni hiyo ni bora kutokana na
uzalishaji wake kukidhi haja na kuwaongezea kipato.
Wamesema unapovuna Mahindi
machache lakini unga unakuwa mwingi tofauti na kiwango hali kadhalika ladha ya
unga wake pamoja na mahindi yenyewe ambayo mara nyingi huishia kuchoma na
kuwaomba wasambazaji kuwaisha Mbegu hizo kwa wakati ikiwa ni pamoja na
kuwatafutia soko la uhakika kutokana na kujikita katika uzalishaji.
Aidha wakulima hao zaidi ya 30
walizawadiwa kila mmoja Kilo mbili za mbegu za mahindi kwa ajili ya mfano ili
wapande na kujionea manufaa na ubora wa mbegu hizo kabla ya kuanza kuuziwa ili
wabadilishe mfumo kutoka kutumia mbegu za zamani na kutumia mbegu za kisasa
zilizofanyiwa utafiti.
No comments:
Post a Comment