Mwenyekiti wa TASO Kanda ya nyanda za juu Kusini Kepten mstaafu Nkoswe akizungumza na waandishi wa Habari nanenane
Mkurugenzi wa Bahari Zoo anaeleta wanyama hai Willy Kusaga Nanenane akizungumza na waandishi wa Habari
Mkurugenzi wa kampuni ya MLM International Vision (T) Limited William Mkandawile akifafanua Jambo
Fisi akiwa tayari katika viwanja vya maonesho
Simba Jike akiwa tayari katika viwanja vya maonesho
Simba Dume akiwa tayari katika viwanja vya maonesho
Waandishi wakipata ufafanuzi wa maonesho ya Nanenane mwaka huu 2013 katika mkutano uliofanyika katika ofisi za TASO Mbeya.
***********
BAADA
ya kiu ya Muda mrefu kwa Wakazi wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini ya kutokuwaona
Wanyama hai kwa zaidi ya miaka 30, hatimaye Maonesho ya Nanenane Mwaka huu
yatakayofanyika Kikanda Mkoani Mbeya Wameletwa.
Wanyama
hao wanaoletwa kwa Udhamini wa Kampuni ya Pepsi na MLM International Vision (T)
Ltd kutoka katika Kampuni inayohusika na Wanyama hai ya Bahari Zoo kutoka
Jijini Dar Es Salaam itatoa fursa kwa Wakazi wa Kanda hii kujionea kwa ukaribu
na kumaliza kiu ya Muda mrefu.
Akizungumza
katika mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika Leo katika Viwanja vya John
Mwakangale Uyole Jijini Mbeya, Mkurugenzi wa Bahari Zoo Willy Kusaga amesema
kwa utafiti wake amebaini kuwa mara ya mwisho wanyama kama Simba, Chui, Chatu,
Mbega, Fisi na wengine walikuja Mbeya Mwaka 1977.
Amesema
yeye binafsi anajisikia fahari kuona Wakazi wa Mbeya walivyoitikia ujio wa
Wanyama hao na kwamba utalii wa Ndani utatangazwa vilivyo na kuhamasisha
Wananchi kuanza kupenda kutembelea vivutio vilivyojirani na makazi yao.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (TASO) Kanda ya Mbeya, Noel Nkoswe
alisema maandalizi ya Nanenane Mwaka huu ni makubwa kutokana na watu
kuham,asika na waoneshaji kuongezeka tofauti na maonesho ya nyuma.
Amesema
hamasa kubwa imetokana na kiu ya kuwaona wanyama kutokana na kutokuwepo kwa
muda mrefu na wengine kukosa fursa ya kutembelea mbuga za Wanyama zilizozoeleka
ikiwa ni sababu za uchumi na umbali.
Ameongeza
kuwa sababu nyingine itakayoleta hamasa ya maonesho ya Mwaka huu ni fursa ya
kuandaa maonesho ya Kitaifa yaliyohamishiwa Dodoma kwa Mwaka wa Sita Mfululizo
hivyo kuwafanya Wananchi kuamini Mwaka huu kufanyika kitaifa Mkoani Mbeya.
Mwenyekiti
huyo amesema katika Uzinduzi wa Nanenane Kwa Kanda hii utafanywa na Waziri Wa
Uchukuzi, Dr. Harisson Mwakyembe ambapo Siku zitakazofuata kila Mkuu wa Mkoa
atapangiwa siku yake kwa ajili ya Mkoa husika kuonesha shughuli za Wakulima
wake.
Alizitaja
siku hizo kuwa ni Agosti 2, Mwaka huu kufanywa na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya huku
Mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, Agosti 3, Mkoa wa
Rukwa, Agosti 4 mkoa wa Iringa, Agosti 5 Mkoa wa Njombe, Agosti 6 Mkoa wa
Ruvuma na Agosti 7 utakuwa ni Mkoa wa Katavi.
Picha na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment