JENGO LA OFISI YA HALMASAHURI YA RUNGWE
Kitendo cha serikali kusogeza madaraka kwa
karibu zaidi na wananchi ili kuwawezesha kuamua mambo yanayo husu maisha
maendeleo ya kila siku imechangia kwa asilimia kubwa baraza la madiwani
halmashauri ya wilaya ya Runwe kuamua kutumia hoja hiyo kuugawa mkoa mbeya na
kuwa mikoa miwili.
Moja ya sababu ambazo zimepelekea baraza hilo
kutumia hoja hiyo kama kigezo mojawapo cha kujipatia mkoa mpya ni pamoja
na kupanga kubuni na kutekeleza kulinda na kuendesha mipango yao kwa
kutekelezwa kitaalamu zaidi katika kuwaletea maendeleo wananchi endapo mkoa huo
utapatikana.
Hatua hiyo imefikiwa katika kikao maalumu
cha baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kilicho keti
kujadili mpango wa ugawaji wa Mkoa wa mbeya kuwa mikoa miwili ambapo katika
katika kikao hicho baraza hilo la madiwani limefikia maamuzi ya kuugawa
mkoa huo wa mbeya na kuuita mkoa wa Rungwe ambapo makao makuu yake
yamependekezwa kuwa Mamlaka ya mji mdogo Tukuyu.
Akiwasilisha mapendekezo ya kamati tendaji( CMT)
na kamati ya fedha Ndugu Noel Mahyenga amesema wanaipongeza serikali ya
awamu hii kwa hatua yake ya kukubali kutoa mapendekezo yake ya ugwaji wa mkoa
wa mbeya kwa lengo la kupunguza mzigo na majukumu Ya serikali kwa lengo la
kuwaletea maendeleo wananchi.
Amesema katika kufanya hayo serikali imekuwa
ikigawa mikoa wilaya na Halmashauri ili kurahisisha utawala na uendeshaji wa
taasisi hizo katika hatua moja wapo ya utekelezaji wa malengo yake
yaliyokusudiwa.
Wamesema kulingana na ukubwa wa eneo na idadi ya watu katika mkoa huo wa mbeya
imekuwa vigumu kwa watumishiwaliopo sekretalieti ya mkoa kusimamia
kikamilifu maendeleo ya mkoa kwa maana ya kutoa ushauri wa kitaalamu pamoja na
kusimamia utekelezaji wa shughuli mablimbali za kimaendeleo kwa wakati muafaka
ili kukidhi haja inayokuwepo wakati inapo hitajika.
Hata hivyo baraza hilo kwa nguvu moja limekubali
kutoa moja ya majengo yake mapya yaliyojengwa ndani ya halimashauri hiyo kuwa
ofisi ya mkoa ambapo ujenzi huo umetumia fedha za ndani pamoja na baraza
hilo pia limependekeza halmashauri ya wilaya ya busokelo iwe wilaya ili kufanya
mkoa kuwa na wilaya nne ambazo ni Kyela,Ileje na Busokelo badala ya wilya tatu
zilizopo hivi sasa.
Pamoja na baraza zima la halmashauri hiyo
kupitisha hoja hiyo ya ugawaji wa mkoa mmoja wa madiwani ndani ya baraza hilo
ndugu Anyimile Mwasakilali Kata ya Kawetere( NCCR) kupinga vikali suala la
ugwaji wa mkoa mbeya kutokana na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazo
ikabili wilaya hiyo.
Moja ya changamoto hizo ni pamoja na kata yake
kuto patiwa ofisi ya Afisa Mtendaji kwa muda mrefu sasa hivyo amehoji juu ya
kuanzishwa kwa mkoa mpaya wakati bado kuna changamoto nyingi hivyo
kitendo cha hatua hiyo kitawabebesha mzigo mkubwa wananchi wake pamoja na
serikali kwa ujumla.
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment