Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, May 13, 2013

MGOMBEA UDIWANI KATA YA IYELA KUPITIA CCM ASINDIKIZWA NA WANACHAMA KWA MBWEMBWE KUCHUKUA FOMU







Richard Shangwi Mgombea kiti cha udiwani kata ya Iyela akikabidhiwa fomu na afisa mtendaji kata ya Iyela Safi Almasi



Richard Shangwi Mgombea kiti cha udiwani kata ya Iyela 





Add caption


CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kata ya Iyela Jiji la Mbeya kimewaahidi wanachama na wananchi wake kutekeleza  na kuyaendeleza mambo mazuri yaliyoachwa na viongozi waliopita ili kujenga imani na Serikali yao ya Chama.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Richard, Shangwi wakati wa hafla ya Uchukuaji wa Fomu ya kugombea Udiwani katika kata ya Iyela kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwani wa kata hiyo, Dominick Tweve aliyekuwa maarufu kwa Jina la  Mzee Nkwenzuru aliyefariki dunia Mwaka jana Agosti 9, Hafla  iliyofanyika katika Ofisi za Afisa Mtendaji wa kata hiyo.
  
Richard alisema Chama chake kimemwamini na kumpendekeza yeye kuwania Udiwani ili akayaendeleze mazuri yaliyofanywa na Diwani aliyepita sambamba na mengine aliyokuwa ameanza kuyafanya na kuishia njiani kabla ya kufikwa na Umauti.
  
Katika uchukuaji wa Fomu hiyo  Richard Shangwi alisindikizwa na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwemo viongozi mbali mbali kama Mwenyekiti wa Chama Wilaya, Katibu Mwenezi Mkoa, Katibu wa UVCCM Mkoa, Ktibu wa Chama Wilaya, Katibu Mwenezi wa Wilaya, Mnec, Mjumbe wa Mkutano mkuu taifa na  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Fomu hizo, Mgombea huyo alisema kama Chama wanategemea kurudisha Fomu Mei 13, Mwaka huu majira ya Saa tano asubuhi ambapo Kampeni kwa ajili ya kunadi Sera za Chama zitazinduliwa Mei 18, Mwaka huu na kutumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kufika kwa wingi katika Mikutano ya Kampeni itakapoanza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi wa kata hiyo ambaye pia ni Afisa Mtendaji wa kata ya Iyela Safi Almasi alisema zoezi la uchukuaji Fomu lilianza kwa kusuasua ambapo rasmi wameanza kuchukua Mei 9, Mwaka huu zoezi ambalo litafikia ukomo Mei 12, Mwaka huu.

Mtendaji huyo aliwataja wagombea waliojitokeza kuchukua Fomu ni kutoka chama cha DP Amos Anyisile Mwambagi, kutoka CHADEMA Charles Changani Mkera na Mgombea wa Chama cha Maapinduzi Shangui J. Richard.
  
Aliongeza kuwa Wananchi kutoka Vyama vyote vya Siasa wajitokleze kuchukua Fomu hizo ili kuendana na muda waliopangiwa kuendesha zoezi la Uchaguzi huo na kuongeza kuwa Kampeni zitaanza Mei 15, Mwaka huu wakati zoezi la uchaguzi na upigaji kura litafanyika Juni 16, Mwaka huu.

Na Mbeya yetu


1 comment:

Msalya said...

Kila la kheri Kaka, ila kwa chama ulikopitia mmhh