Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, May 13, 2013

MAADHIMISHO YA WAUGUZI DUNIANI YAFANA MBEYA

Wauguzi wa Hospitali ya mkoa Mbeya wakiandamana kuelekea wodini kuwapa zawadi wagonjwa 
Katibu wa Afya Mkoa wa Mbeya, Juliana Mawala ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo alitoa zawadi mama aliejifungua mtoto katika hospitali hiyo ya mkoa wa Mbeya 
Wauguzi mbali mbali walijumuika na mgeni rasmi katika kutoa zawadi kwa wagonjwa kuwaonyesha upendo na kuwajali wagonjwa wao
Wagonjwa wakifurahia kupata zawadi toka kwa wauguzi
Washa taa washa taa washa taa ya upendo wauguzi


Naapa mbele za Mungu na Mbele ya Mhadhara huu, kuendesha maisha yangu na kutekeleza wajibu wa kazi zangu kwa udhu na uaminifu nitaacha kufanya vitendo vyovyote vile vilivyo viovu na sitachukua dawa yoyote ile ninayoifahamu kuwa ina madhara, nitafanya kila ninoaloweza kwa nguvu zangu zote ili kuimarisha na kuinua hadhi ya uuguzi” na kuongeza kuwa,

Nitatunza kwa uthabiti siri nizipatazo ziwe za wagonjwa,familia au vinginevyo ambazo nitazifahamu kwa wajibu wa wito wangu kwa uaminifu, tutasaidiana na daktari katika katika kumhudumia mgonjwa nitajitolea kuwahudumia wote wanaohitaji huduma zangu” walisema Wauguzi hao wakila kiapo.







IMEELEZWA kuwa Uuguzi na Ukunga ni taaluma muhimu yenye mchango mkubwa katika kuboresha huduma za Afya nchini, ambapo wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, taratibu na miongozo ya kazi zao.


Aidha wauguzi na wakunga wametakiwa kufuata miongozo ya kitaaluma iliyowekwa na kuthamini, kuheshimu uhai wa wa watejwa ambao ni wagonjwa bila kujali uchumi wa mtu, rangi, kabila au ugonjwa alionao kwa kuongozwa na misingi ya maadili ya Uuguzi na Ukunga.

Hayo yamesemwa na  Katibu wa Afya Mkoa wa Mbeya, Juliana Mawala  katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyka katika hospilatali ya mkoa alisema Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka imekuja katika muda mwafaka ambayo  inasema “Kuziba Mapengo kufikia malengo ya millenia namba   4,5 na  6.” 


Mawalla alisema  kuwa dunia ipo kwanye mapambano dhidi ya vifo vya mama na Mtoto vitokanavyo na sababu ambazo zinaweza kuzuilika endapo wauguzi watajikita zaidi katika kutekeleza maazimio ya malengo ya milenia zilizotajwa.

Alisema  maadili ya Uuguzi ndiyo dira na Mwongozo wa dhana ya uuguzi kwa wauguzi wote nchini ,Hivyo mnapaswa kuzingatia maadili ya Uuguzi, huku mkitekeleza maagizo ya sera na  Miongozo mbalimbali itolewayo na Baraza la Uuguzi na Ukunga pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.

Aidha Katibu huyo alikili uwepo wa  wauguzi wachache  ambao wamekuwa na tabia ndogondo zisizoendana na Maadili ya Uuguzi, ambapo alitoa wito kwa Wauguzi kushirikiana kuwakemea na kuwafichua  pale inaposhindika ili wauguzi hao wachache wasiharibu Fani hii nzuri ya Uuguzi.

Pia aliwaasa wauguzi kutekeleza wajibu wake katika kupambana na Janga la Ukimwi  na kuongeza kuwa wasipime Virusi Vya Ukimwai kwa macho na kudhani kuwa mtu mwenye Afya Nzuri hajaambukizwa bali watumie vipimo vilivyodhibitishwa kitaalamu.

“Ndugu Wauguzi , napenda kuwahamasisha na kuwasisitiza juu ya umuhimu wa kuwa kitu kimoja na kushirikiana katika kuboresha na kukuza chama chenu kwa kuhakikisha kuwa kila muuguzi ni mwanachama na anashirikiana na wenzake katika michango mbalimbali kwani mahali penye chama ndipo panapoweza kuwaunganisha watu na wakaweza kuwa na nguvu ya kuongea kwa kauli moja , hivyo viongozi lisimamieni hilo nasisi  tunaahidi tutakuwa  pamoja nanyi ii kuhakikisha chama chenu  kinakuwa imara” alisisitiza Katibu huyo.

Aliongeza kuwa  katika huduma za afya apewazo mgonjwa, Muuguzi hutoa  theluthi mbili ya huduma zote azipatazo mgonjwa  na tunakiri kuwa Hospitali bila Muuguzi haitaweza kuitwa hospitali  hivyo basi kuweni mifano bora katika utoaji wa huduma za Afya, kuweni wabunifu Muwahudumiapo wagonjwa na kuweni watetezi na washauri wa wataalamu wengine katika kumhudumia mgonjwa.

Na mbeya yetu

No comments: