Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, April 24, 2013

Wito umetolewa kwa wananchi mkoani mbeya kuhakikisha wanaendelea kuilinda na kutetea amani iliyopo badala ya kukubali kupandikizwa chuki na baadhi ya watu wasio utakia mema mkoa na Taifa kwa ujumla.




Wito umetolewa kwa wananchi mkoani mbeya kuhakikisha wanaendelea kuilinda na kutetea amani iliyopo badala  ya kukubali kupandikizwa chuki  na baadhi ya watu wasio utakia mema mkoa  na Taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa  Scourt Mkoa wa mbeya Ndugu Pablo Sanga akizungumza na waandishi wa habari jijini humo amesema kuwa kuna kila sababu ya wananchi mkoani humo kuilinda amani ya mkoa huo ilikuvutia shughuli za kimaaendeleo .

Amesema katika kipindi cha hivi karibuni  kumekuwepo na matukio mbalimbali yanayoashiria kuvuruga amani ya mkoa huo hivyo nivema wananchi wa mkoa huo wakawa makini na baadhi ya watu wanaopandikiza chuki  zidi ya viongozi wao na serikali yao kwa ujumla.

Pablo amesema siasa chafu zinazo enezwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini ndizo zitakazo weza kusababisha madhara ambayo ndiyo yatakayo changia kuvuruga kwa amani ambayo imedumu kwa muda mrefu sasa.
Kauli hiyo ya kiongozi wa scourt mkoani humo imekuja kufuatia kuwepo kwa ujio wa kiongozi wa kitaifa Rais Kikwete ambaye anatarajiwa kufanya ziara ikiwa ni pamoja na kuzungumza katika sherehe ya mei mosi kitaifa ambayo itafanyika mkoani hapa.

Hata hivyo Kiongozi huyo wa Scourt amesema wamejipanga vyema kuhakikisha wanampokea vyema Raisi Kikwete katika kuhakikisha kuwa kiongozi huyo anafanya ziara yake  kwa amani na utulivu bila kuwepo kwa vitendo viovu.


No comments: