Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, April 29, 2013

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za siku ya wafanyakazi duniani Mei mosi itakayofanyika kitaifa Mkoani Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbasi Kandoro akizungumzana waandishi wa habari ofisini kwake amesema Raisi Kikwete anatalajiwa kuwasiri mkoani hapa Apri 30 mwaka kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa songwe majira ya saa4 na Nusu asubuhi.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya wakimsikiliza mkuu wa mkoa MbeyaRais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za siku ya wafanyakazi duniani Mei mosi itakayofanyika kitaifa Mkoani Mbeya.

Pamoja na kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo pia anatarajiwa kuzungumza na wakuu wa shule na Wamiliki wa Vyuo binafsi ( katika ukumbi wa mkapa Apri 30 mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbasi Kandoro akizungumzana waandishi wa habari ofisini kwake amesema Raisi Kikwete anatalajiwa kuwasiri mkoani hapa Apri 30 mwaka kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa songwe majira ya saa4 na Nusu asubuhi.

Amesema mara baada  ya kuwasili mkoani hapa atazungumza na wamiliki wa shule hizo ambao alitajiwa kuzungumza nao Aprii 29 mwaka lakini ikashindikana kutokana na kuwepo kwa mkutano wa viongozi nchi za Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.

Amesema mara baada ya kuingiliana kwa ratiba hiyo baadhi ya ratiba ambazo zilitarajiwa kufuatwa zimevunjwa hasa zile za uzinduaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo hasa katika Wilaya ya Rungwe,Mbarali,Mbozi ambapo Mweshimiwa Rais Kikwete anatalajiwa kufanya ziara nyingine kwa ajili ya shuhuli hizo hapo baadae.

Kutokana na hali hiyo Mkuu huyo wa Mkoa amesema mara baada ya kuzungumza na wakuu wa shule pamoja na viongozi wa chama cha wafanyakazi( Tucta)ambapo baada ya hapo atapokea taarifa ya mkoa pia  kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha Mei mosi ambapo jioni atalejea jijini Dar es salaam kuendelea na vikao vingine. 

Pia katika taarifa yake kwa waandishi wa habari jijini hapa Kandoro amewaomba radhi wananchi wa mkoa wa mbeya ambao walijiaanda kwa lengo la kumpkea kiongozi wao kutokana na kusitishwa kwa tatiba hizo.

Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa wa Mkoa wa mbeya Ndugu Abbasi Kandoro amewataka wananchi wa jiji hilo la mbeya kujitokeza kwa wingi kumraki Mheshimiwa Rais mara atakapo wasiri jijini Mbeya katika uwanja wa kimataifa wa Sonwge( SIA) pamoja na kujitokeza kwa wingi katika sherehe za Meimosi kitaifa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa.

3 comments:

Maria - Nonde Mbeya said...

Asante kwa habari nyingi tunazozipata kupitia Mbeya yetu, Ushauri wangu ni kwamba makosa ya maneno yawe yanahaririwa kabla ya kuandika kwenye blog, kwa mfano ujio wa Rais maneno mengi yamekosewa. mfano Raisi, Kumpkea,Sonwge n.k
Asante