Michuano ya mei mosi kitaifa katika uwanja wa kumbukumbu sokoine
jijini mbeya imeendela kushika ambapo hii leo michezo mbalimbali imefanyika
uwanjani hapo baada ya kufunguliwa
rasmi na mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa mbeya Ndugu Costantine Mushi.
Katika michezo ya awali kwa upande wa wanaume ilikuwa ni kati ya
Wizara ya Mambo ya ndani pamoja na Wizara ya Mali asili.
Matokeo ya mchezo huo Timu ya Mambo ya Ndni imefanikiwa kuibuka
kidedea kwa kuicharanga goli 3 kwa mbili timu pinzani.
Katika dk ya 22 maliasili walifanikiwa kuandika bao la kwanza kupitia
kwa mchezaji wao Hamisi Changánda mara baada ya kupkea pasi kutoka wingi ya
kulia.
Katika kpindi hicho cha
kwanza wapinzani wao ambao ni Mambo ya ndani walisawazisha bao hili katika dk 38
kwa mchezaji westoni mwanjala kwa kichwa ambapo mpaka mchezo huo unakamilika
katika kipindi cha kwanza timu
zote zilikwenda suruhu.
Hata hivyo kipindi cha pili mpambano ulikuwa mkali kwani timu zote
zilikuwa na kasi kubwa kwani dk ya .47 Andrew Bundara wa mambo ya nadani
aliandikia timu yake bao la pili ambapo katika dk ya 60 Hamisi Nyagawa aliipachikia timu yake
ya Maliasili bao la kusawazisha.
Mambo ya ndani waliendela kulindama lango la wapinzani wao na
kufanikiwa kuandika bao la 3 na la ushindi kupitia kwa mchezaji wao hatari
Westoni Mwanjala ambaye nfdite aliyekuwa kinara wa mapmbano huo kwa kuiandikia
timu yake ya mambo ya ndani bao 3 katika kipindi chote cha dk 90 za mchezo.
Michezo mwingi ne wa pete kati ya CDA ya Dodoma pamoja Hazina Dar es
salaam matokeo ni ,,,,,,,,,,,,CDA 31 Hazina 12…………Ulinzi ya Dar 38 Uhamiaji 17
.
Katika mchezo wa kuvuta kamba Hazina wanaume walishindwa nguvu na
Uhamiaji.
|
2 comments:
Jamani, uwanja wa sokoine ufanyiwe ukarabati, unatia aibu jamani kwa jiji kubwa kama Mbeya. Wadau lioneni hilo
naomba picha zaidi na pia naomba toa taarifa za kila siku za michezo hadi siku ya kufunga nakutegemea wewe
Post a Comment