WANANCHI wa
kitongoji cha Mkulila kijiji cha Wambishe kata Ulenje wilaya ya Mbeya Mkoani
hapa wamekataa mradi wa umwagiliaji uliopelekwa na serikali kwa madai kuwa
hawakushirikishwa wakati wa uanzishwaji wa mradi huo ambapo pia wamesema
hawaoni faida ya kuwa na mradi kama huo kijijini hapo.
Mradi
ni kwa ajili ya umwagiliaji ulioletwa na serikali kwa gharama ya shilingi zaidi
ya milion 40 ambapo wananchi hao wamedai kuwa mradi wa maji hautawasaidia
chochote kutokana na kuwepo kwa mfereji unaotiririsha maji kwa kipindi chote
cha mwaka.
Hayo
yamebainishwa na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini
hapo ulioitishwa na Ofisi ya Wilaya kwa lengo la kuwaelimisha wananchi hao juu
ya faida ya mradi huo jinsi utakavyowanufaisha kama kijiji na wananchi kwa
ujumla.
Pamoja
na Maofisa hao kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa mradi walipinga
vikali huku wakidai fedha za meadi huo zipelekwe sehemu nyingine zakafanye kazi
zingine.
Mkutano
huo uliokuwa ukiongozwa na Maofisa Umwagiliaji kutoka Ofisi ya Halmashauri ya
Wilaya ya Mbeya ambao ni Malonga Msuya na John Kajange walijikuta katika wakati
mgumu kutokana na mwitikio hafifu wa wakazi.
Hata
hivyo Diwani wa kata hiyo Noel Mwankwale amewasihi wananchi hao kuwa wasikivu
na kuukubali mradi huo lakini pia juhudi zake ziligonga ukuta baada ya wakazi
hao kuendelea kusisitiza kuwa hawautaki kabisa.
Wamesema
fedha hizo ni nyingi na kwamba haziwezi kutumika kujengea mfereji ambao hauna
tatizo walamanufaa kwao kutokana na kutiririsha maji muda wote.
Miongoni
mwa watu waliozungumza katika mkutano huo na kuukataa mradi ni pamoja na chifu
wa eneo hilo Michael Mwaifwani ambaye amesisitiza kuwa yeye kama chifu hajaona
tatizo lolote katika mfereji huo.
Mmoja
wa wakazi hao Christian Matengere ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho
aliyeondolewa alisema ni vema wananchi wakasikilizwa na kutendewa vile
wanavyotaka na siyo kuwalazimisha.
Amesema
pia anasikitika kuona Serikali kutorudisha fedha zake alizokuwa ametoa
kwa ajili ya kufungua akaunti ya benki kwa ajili ya mradi huo ambao alisema
hauna maana yoyote.
Awali Maofisa hao
wamesema lengo lao la kufika kijijini hapo ni kutoa elimu ambayo walikuwa
wakiilalamikia kwamba hawakuipata kuhusu mradi na manufaa ya mfereji na kwamba
hakuna shamba wala nyumba itakayoathirika wakati wa ujenzi wa mradi huo.
Aidha Mkutano huo
ulifungwa pasipo kufikia muafaka wowote licha ya wananchi kuendelea
kusisitiza kutouhitaji na kushauri kuwa mradi huo upelekwe kijiji cha jirani
che uhitaji wa maji na sio wao.
|
No comments:
Post a Comment