Mhasamu
askofu wa katoriki jimbo Mbeya Ask. Evaristo Chengura
WANAFUNZI wa vyuo
vikuu ambao ni waumini wa dhehebu la Katoliki mkoani Mbeya wamedai kuwa
wamekukipambana na changamoto ya ushawishi wa kujihusisha na ushoga vyuoni
kwao.
Wakisoma risala yao mbele ya
Mhasamu askofu wa katoriki jimbo Mbeya Ask. Evaristo Chengura katika semina kwa
muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu waumini wa Katoriki
Mbeya (MUCCASA), walisema kuwa wamekuwa wakikabiliana na changamoto ya ushoga
vyuoni.
Akisoma risala hiyo
Mwenyekiti wa Muccasa, Alfred Nditi alisema kuwa wamekuwa wakikabiliana na
changamoto ya uhamasishwaji wa masuala ya ushoga unaoshawishiwa na mataifa
makubwa ya ughaibuni.
Alisema ushawishi huo
umekuwa ukiwalenga vijana hasa walio katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu
hapa nchini ili wajikite katika uovu huo.
“Ushoga umekuwa
ukihamasishwa na mataifa mbalimbali hasa yale makubwa ya Ughaibuni na
ukitulenga vijana tulio kwenye vyuo vikuu hapa nchini,” Alisema Nditi.
Alisema ili kupambana na
changamoto hizo wanamatarajio ya kupinga ushoga kwa kauli moja ili kukidhi
dhana ya Mungu na uumbaji wake.
Nditi aliongeza kuwa
upingaji wa ushuga utakuwa ni wa kauli moja kwa wanaMuccasa na kuhakikisha
dhana ya Mungu ina heshimiwa na thamani ya binadamu ienziwe.
Naye Askofu Chengula alisema
kuwa ushoga umekuwa ukipingwa sana na viongozi wote wa dini lakini umekuwa
ukiendeshwa chini chini na baadhi ya watu.
“Ushoga unapigiwa sana
kelele lakini kumekuwa na watu wanaouendesha chini kwa chini na kwa siri kubwa
katika maeneo mbalimbali na hasa katika vyuo,” alisema Ask. Chengula.
Aliwaasa wanamuccasa kwu
kuwaonya wale watakao wakuta wanakijihusisha na mambo hayo machafu na
kuwashawishi kuachana na matendo hiyo.
Alisema ni vema wakawapatia
elimu juu ya kuachana na mambo hayo na kuwaeleza madhala na ubaya wa Ushoga
katika maisha yao kwani wengine wanakuwa wameathirika kisaikolojia.
Semina hiyo kwa wananchuo
ililenga kuwaelimisha wanachuo hao juu ya imani yao na jinsi ya kusimama katika
imani ambapo ilihuzuriwa na wanachuo kutoka katika vyuo mbalimbali vya Mkoani
Mbeya.
Muccasa ni muunganiko wa
wanachuo kutoka katika vyuo vikuu na taasisi za Mkoani hapa na inajumla ya
matawi 20 ya wanamuccasa.
Kwa hisani ya Furaha Elimitaa blog
|
No comments:
Post a Comment