HALMASHAURI
ya Jiji la Mbeya limelazimika kuifuta Sheria ndogo ya Halmashauri hiyo namba
376 (4)na (1) ya Mwaka 2011 iliyokuwa inataka kusajili magali ya kukodi,
teksi,Bajaji na Pikipiki kwa kulipia ushuru Shilingi 58,000/=kwa Mwaka.
Sheria
hiyo imefutwa baada ya kutokea
ugomvi mkubwa baina ya wamiliki na madereva wa magari kuanzia tani moja hadi
tano nne na wakala aliyepewa zabuni ya kukusanya ushuru huo.
Ushuru
unaolalamikiwa na wamiliki hao wa magari ni ule unaokusanywa na Halmashauri
hiyo kupitia kwa wakala aliyejulikana kwa jina la Mbuzax Auction Mart &
Court Brockers inayomilikiwa na Emmanuel Mbuza.
Wananchi
hao walitoa malalamiko hayo kwenye mkutano wapamoja kati ya wamiliki wa magari,
madereva na viongozi wa Halmashauri ya Jiji chini ya Meya uliofanyika katika
ukumbi wa Halmashauri uliopo Sokomatola Jijini hapa.
Wakizungumza
kwenye mkutano huo Madereva hao wamesema utaratibu wa ushuru huo unawaumiza
sana kutokana na kuwa na gharama kubwa kama ushuru wa usajili kwa mwaka
Shilingi 58,000/= pamoja na ushuru wa kuegesha magari kila siku shilingi
1000/=.
Paulo
Mwasilelwa Dereva wa Pick up ambaye pia ni katibu wa Chama cha waendesha maroli
Jiji la Mbeya amesema wanapingana na ushuru huo ambao unatozwa unawaumiza kwa
sababu hulazimika kulipia gharama za usajili wa gari linaponunuliwa, bima ya
gari,Tra, maegesho na zimamoto ambavyo lazima vilipiwe.
Amesema
Kodi ya Maegesho ni zaidi ya Shilingi 360000 kwa mwaka hivyo ukiongeza na
ushuru wa usajili gari haliingizi fedha yoyote badala yake linadumaza uchumi wa
mwananchi wa kawaida ambapo aliongeza kuwa biashara ya magari hiyo haina
uhakika kutokana nakutokuwa na wateja wanaoeleweka badala yake wanasuburi
kukodishwa.
Wameongeza
kuwa utaratibu unaofanywa na wakala huyo ni mbovu ambao walidai kuwa wakala
huyo hutumia nguvu nyingi hali inayosababisha kuhatarisha maisha yao kutokana
na watumishi wa wakala huyo kutumia mapanga kuwatishia maderev pamoja na
kuwajeruhi.
Akijibu
tuhuma hizo Meya wa Jiji la Mbeya Ndugu
Attanus Kapunga aliyekuwa amefuatana na Kamati ya Fedha ya baraza la
madiwani wa Halmashauri hiyo alisema kutokana na sheria iliyokuwa imepitishwa
na madiwani hao kutotolewa elimu kwa wananchi wanaotakiwa kulipa kodi
inamakosa.
Kapunga
amesema kama sheria haileti amani baina ya wananchi inatakiwa iangaliwe upya
hivyo wakala anatakiwa kusimama mara moja ili Sheria hiyo iangaliwe upya kwa
maslahi ya maendeleo ya Jiji hilo.
Amesema
kitendo cha wakala huyo kukusanya ushuru kinyume na maeneo aliyoaambiwa ni kosa
kubwa ikiwa ni pamoja na kutumia ubavu kudai kodi ambayo Halmashauri haijamtuma
ni kinyume na taratibu alizopangiwa.
Ameongeza
kuwa kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kwenye sheria hiyo lazima wakala
asimame asubiri vikao vikae upya na kuitazama upya ili isiwagombanishe na
wananchi hali itakayosababisha uvunjifu wa amani.
kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbuzax Emmanuel Mbuza ambaye awali
hakupewa nafasi ya kujitetea kutokana na madereva kumzomea pindi aliponyoosha
mkono akitaka kujitetea hadi mkutano unafungwa aliwaambia waandishi wa habari
kuwa anaishukuru Halmashauri hiyo kwa kugundua mapungufu ya sheria zao.
Mbuza
amesema kutokana na kuvunjwa na kufutwa kwa sheria hiyo kutampunguzia yeye
kufanya kazi katika mazingira magumu yanayosababisha kuwa na ugomvi na wananchi
wanaotakiwa kulipia ushuru huo.
Amesema
kilichofanyika ni Hlmashauri ya Jiji kugundua kuwa sheria iliyokuwa ikitumika
ilikuwa na mapungufu ambayo wakala asingeweza kuyajibu badala yake walipa kodi
walikuwa wakitoa lawama ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake.
|
No comments:
Post a Comment