Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, March 27, 2013

NWAKA MWAKISU AKONGA NYOYO ZA VIJANA MBEYA

Nwaka Mwakisu akiongea na vijana wa Uyole hivi karibuni 
Diwani wa Kata ya Itezi Frank Maemba amesema wanachokifanya Vijana hao ni kutekeleza sera za chama cha mapinduzi inayotaka Vijana waunganishwe kwenye makundi ili iwe rahisi kupatiwa misaada ikiwa ni pamoja na kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana.
Timu ya Redio  Bomba fm, 
Timu ya  Veterani ya Uyole 
Timu mbali mbali zilikuwepo uwanjani hapo
Vijana mbali mbali walijitokeza kuchangia damu siku hiyo


BAADHI ya Wananchi na wakazi wa Mkoa wa Mbeya wamepongeza jitihada za Vijana wanaojitolea kusaidia makundi ya watu wasiojiweza na wenye uhitaji kutokana na kufanya hivyo bila kujali itikadi za vyama  wala dini zao.

Kijana anayetajwa kukonga mioyo ya wananchi wa Mbeya kutokana na kusaidia makundi mbali mbali ya Vijana, Yatima na wazee ni Mjumbe wa Mkutano mkuu Taifa kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Nwaka Mwakisu.
  
Wananchi hao wamesema Nwaka Mwakisu amekuwa kivutio kwa Vijana wengi wa kada mbali mbali kutokana na ushiriki wake katika kazi za maendeleo ndani ya Mkoa wa Mbeya ambapo pia amekuwa akiwaunganisha vijana hao kwenye makundi ili waepukane na shughuli zisizofaa katika jamii.
  
Wamesema Mwakisu ameonesha moyo wa tofauti miungoni mwa Vijana Mkoani Mbeya ambapo katika kipindi kifupi cha kuanzia Januari hadi Machi Mwaka huu ameshiriki na kuambatana na vijana kutembelea vituo vya watoto yatima vilivyopo Uyole na Simike Jijini Mbeya.
  
Wakizungumza na Mbeya yetu katika mahojiano maalumu juu na namna Vijana wenye  uwezo wanavyoweza kusaidia makundi mbali mbali katika kuwakomboa kiuchumi  ambapo hawakusita kumtaja Nwaka Mwakisu kuwa ni miongoni mwa vijana wachache wanaojitolea kwa moyo wote.
  
Iddi Ramadhani ni Mwenyekiti wa Bajaji Jiji la Mbeya ambaye alisema Mwakisu amewatembelea mara kadhaa katika kujua wanahitaji nini ili aweze kwasaidia ambapo ameshwasaidia vijana hao Vifaa vya michezo kama vile Jezi, Soksi na Viatu kwa ajili ya timu ya Waendesha bajaji yenye makao makuu Ilemi Jijini Mbeya.
  
Mbali na waendesha bajaji vijana wengine walionufaika na Msaada wa Mwakisu ni timu za Mpira kutoka Uyole katika kata ya Itezi Jijini Mbeya ambao walipatiwa vifaa vya michezo ambavyo ni seti tatu za Jezi na mipira kwa ajili ya mashindano ya Umoja yaliyomalizika hivi karibuni.
  
Nwaka Mwakisu alipotafutwa kuzungumzia maswala hayo alisema binadamu tumeumbwa kwa ajili ya kusaidiana hivyo si vibaya kwa yeye kujitolea kwa watu wenye uhitaji ambapo aliongeza kuwa hafayi hivyo kwa ajili ya kujinufaisha yeye binafsi.
  
Alisema kiu yake ni kuona Vijana wanakuwa na umoja kwani baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwatumia vijana kuvuruga amani Mkoani Mbeya ambapo baada ya vurugu viongozi hao hawajitokezi kuwasaidia pindi wanapopata madhara kutokana na athari wanazopata katika vurugu hizo.


Kutokana na kuwaunganisha vijana hao katika baadhi ya michezo ambapo vijana hao hupata nafasi pia ya kuchangia damu kutokana na uhitaji wa damu katika michezo iliyomalizika Uyole Jijini Mbeya katika viwanja vya Shule ya Msingi Gombe iliyowahusisha timu ya kituo cha Redio cha Bomba fm, Veterani ya Uyole na vijana wengine.


Mbali na vijana hao kumpongeza Nwaka Mwakisu kwa kujitolea na kuwaunganisha Vijana hao, Diwani wa Kata ya Itezi Frank Maemba alisema wanachokifanya Vijana hao ni kutekeleza sera za chama cha mapinduzi inayotaka Vijana waunganishwe kwenye makundi ili iwe rahisi kupatiwa misaada ikiwa ni pamoja na kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana.
  
Hata hivyo wajibu huo umeonekana kutekelezwa zaidi na viongozi vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya ambao wameonekana kuunga mkono juhudi hizo ambao ni Mjumbe wa Mkutano mkuu taifa(CCM), Charles Mwakipesile ambaye aliwahi kutoa Kompyuta yenye thamani ya Shilingi Laki tano na Nusu(550,000/=) kwa  Vijana wanaoendesha Bajaji Jiji la Mbeya.




No comments: