Zahanati ya kijiji cha Malangali ambayo mwanafunzi huyo alikuwa akipima na sasa ameamua kuikwepa zahanati hiyo kukwepa mkono wa sheria
** Kufuatia sakata hilo Diwani viti maalumu atishiwa kuuwawa
** Polisi waingilia kati sakata hilo
Mkazi wa Kijiji cha Mpona Kata ya Totowe Wilaya
ya Chunya Mkoani Mbeya anatuhumiwa kumwachisha masomo mwanafunzi wa kidato
cha pili katika Shule ya Sekondari Totowe kwa kumuoa
kisha kumpa ujauzito.
Mwananchi huyo aliyefahamika kwa jina la Ndugu
Shigala Mwachanya anatuhumiwa kutenda kosa hilo kwa kumpa ujauzito
mwanafunzi aliyejulikana kwa jina la Ngolo Jiguma(19) ambaye amesitisha masomo
yake kutokana na ujauzito alionayo ambapo wazazi walipatana kulipana Ng’ombe 45
kama fidia ambapo tayari Ng’ombe 20 wameshatolewa.
Aidha kutokana na Mwanafunzi huyo kutambua
kuwa Wazazi wake wametenda kosa ameamriwa kuto hudhulia kliniki katika
kituo cha afya cha Malangali na badala yake amekuwa akienda katika Zahanati ya
Totowe ili kukwepa kukutwa na vyombo vya sheria.
Uongozi wa Kijiji hicho umeanza
kulifuatilia sakata hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkuu wa Shule
aliyokuwa akisomaMwanafunzi huyo Frank Mwakisyala ambapo juhudi hizo
zinaonekana kugonga ukuta kutokana na kutishiwa kuawa na mtuhumiwa.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji
hicho Ndugu Yaledi Mwanguku amesema kuwa suala hilo lipo juu
ya uwezo wake hivyo alilazimika kulipeleka suala hilo kwenye uongozi wa kata
kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Diwani wa Viti Maalumu kata hiyo Christina
Kibwana ambaye alionekana kulipokea suala hilo na kuanza kulifuatilia pia
alidai kuwa alipokea ujumbe mfupi wa maandishi ukimtaka ahame kijijini hapo
lasivyo aache kulifuatilia sakata hilo na asipoacha angeuawa.
Diwani huyo amesema ujumbe huo wenye maneno ya kutishia
yalikutwa kwenye barua nje kidogo nje ya nyumba yake ambapo aliongeza kuwa
baada ya kuona hali hiyo aliamua kutoa taarifa katika kituo kidogo cha
Polisi cha Galula Wilayani Chunya.
Diwani huyo ameendelea kulalamika kuwa baada ya
kutoa taarifa katika kituo hicho hakuna dalili wala hatua zozote
zilizochukuliwa ambapo alisema kuna dalili za Rushwa ambayo inasemekana kuwa
Polisi walipewa Rushwa ya Shilingi Milioni Moja na Nusu(1500,000/=).
Amesema kutokana na kutoonekana kwa hatua zozote
aliamua kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Chunya ambapo
walimkamata mtuhumiwa huyo kisha kufunguliwa kesi katika Mahakama ya Wilaya ya
Chunya.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Totowe kupitia
Chama cha Mapinduzi, Godian Wangala amethibitisha kutokea kwa matukio
yote hayo na kuongeza kuwa amesikitishwa na kitendo cha Mwananchi huyo pamoja
na wazazi kwa kumwachisha masomo na kumsababishia Mwanafunzi kumnyima haki ya
kupata elimu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani
Athumani amekiri kupokea taarifa hizo na kuahidi kulifanyia kazi kwa
ukaribu zaidi na kuhakikisha wahusika watachukuliwa hatua zinazostahili.
Na E . Kamanga Chunya Mbeya
|
No comments:
Post a Comment