WAZIRI wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel
Nchimbi amecharuka na kuwasimamisha kazi maofisa watano wa Jeshi la Polisi
nchini na kuagiza wafuguliwe kesi mara moja katika mahakama ya Jeshi.
Alisema katika tukio la kwanza
lililotokea mkoani Mbeya mwaka jana maofisa watatu wamesimamishwa kazi na
kutarajiwa kufunguliwa kesi kutokana na kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya
kokein.
Alisema baada ya kukamatwa na kwenda
kuifadhiwa katika boahari ya dawa ilipofika kwa mkemia mkuu iligundulika ni
sukari na chumvi
"Tume iliyoundwa kuchunguza
tukio hilo ilibaini kuwa kilichokamatwa na kilichopelekwa kwa mkemia mkuu ni
vitu viwili tofauti " alisema Nchimbi.
Alisema katika tukio hilo aliyekuwa
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi- Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mbeya Eliasi Mwita,
aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi wa mkoa huo Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi Jacob Kiango na aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia, Mrakibu
Msaidizi wa Polisi Charles Kinyongo wamesimamishwa kazi.
Dk. Nchimbi ametoa mwito kwa maofisa wa jeshi la polisi
kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria za jeshi hilo na atakayeenda
kinyume atachukuliwa hatua stahiki.
Kwahisani ya Dotto Mwaibale
|
No comments:
Post a Comment