Mtoto Linah akiwa darasani
SIKU chache baada ya Mbeya yetu kuripoti
habari kuhusu watoto wenye ulemavu wa Ngozi (Albino) waishio vijijini
kutelekezwa bila kupatiwa misaada, Hatimaye majibu yamepatikana baada ya
wahusika kujitokeza na kuwapatia mafuta.
Watoto hao ambao walikuwa na uhitaji wa mafuta ya
kupaka kwa ajili ya kutunza ngozi zao pamoja na miwani na kofia hatimaye wamepatiwa msaada wa mafuta yenye
thamani ya Shilingi Elfu Sitini(60,000/=).
Akikabidhi msaada wa mafuta hayo ambayo huzuia
mwanga wa jua usiumize ngozi zao yaitwayo SunStop 30 ulikabidhiwa na Katibu wa
Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, William Simwali kwa baba mzazi wa watoto
wenye ulemavu wa ngozi.
Katibu huyo alisema mafuta aliyotoa yanatakiwa
kutolewa bure kwa wenye mahitaji ambapo aliongeza kuwa kila yanapoisha
wanatakiwa kutoa taarifa ili waweze kupatiwa mafuta hayo kwa ajili ya usalama
wa ngozi zao ili isishambuliwe na mwanga wa jua.
Kutokanana msaada huo, Katibu huyo alitoa Vichupa
vitano kwa ajili ya watoto wawili wanaosoma katika shule ya Msingi Motomoto
iliyoko katika Kata ya Ruiwa Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa.
Simwale alisema Changamoto wanayokabiliana nayo
ni namna ya kuwafikia Albino kule waliko kwa ajili ya kuwapatia vifaa na
mahitaji yao kutokana na kutokuwa na usafiri ambapo wengi wao hawakai eneo moja
hivyo inakuwa vigumu kuwafikia.
Alisema kutokana na changamoto ya usafiri
inayowakabili wamekuwa wakiwatumia Maofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ambao
hupewa dawa kulingana na idadi ya Albino katika Wilaya yake lakini wamekuwa wakishindwa
kurudisha majibu kama walifika na kukabidhi dawa hizo kwa wahusika.
“ Maofisa maendeleo ya jamii wa kila wilaya ndiyo
tunaowapa dawa hizo lakini tatizo hawaturudishii mrejesho wanapokuwa wamefikia
na idadi ya Albino wanayokuwa wamewapatia” alisema katibu huyo.
Aliongeza kuwa alipojaribu kufuatilia kwa maofisa
hao alibaini kuwa hawapeleki kabisa kutokanana yeye mwenyewe kutoletewa kutoka
katika Wilaya yake ambayo anayehusika anakuwa amekabidhiwa na kuahidi
kulipeleka kwa wahitaji.
Alisema alipojaribu kuwauliza wahusika kwa
kutofika kwa wakati kupeleka mafuta hayo ambayo husaidia kuimarisha ngozi za
walemavu lakini wameishia kudai kuwa hawana bajeti wala usafiri kwa ajili ya
kufanya shughuli hiyo.
Mbali na hilo katibu huyo aliongeza kuwa katika
Shule zote ambazo Albino wanasoma Walimu na wasimamizi waelewe kuwa wanafunzi
hao wanatakiwa kuvaa suruali ili mradi inaendana rangi na sare ya shule husika
kwa ajili ya kuzuia mwanga wa jua ambao huharibu sana ngozi.
Pia alisema hata kwenye maandishi ya kawaida
waowanatakiwa kukuziwa kutokana na kuzaliwa wakiwa na uwezo mdogo wa kuona
ikiwa ni pamoja na kuwapa kipaumbele cha kukaa sehemu ambayo anaweza kusoma
vizuri na kuwa jirani na ubao.
Simwali alisema katika Mkoa wa Mbeya wenye Albino
263 katika kata 114 kati ya kata 217 kwa Mkoa mzima wanahitaji msaada wa hali
na mali kutoka kwa wasamalia wema kwa kuwapatia misaada kama Miwani, kofia na
mafuta.
Alisema Wilaya ya Mbozi ndiyo inayoongoza kwa
kuwa na Albino wengi ambao ni 72, Rungwe 52, Kyela 16, Chunya 35, Mbeya Jiji
19,Mbarali 16, Mbeya Vijijini 48 na Ileje 8 kutokana na Takwimu iliyofanyika
Mwaka 2011.
Kwa upande wake Mzazi wa watoto wenye ulemavu wa
Ngozi Usaje Mwambije, aliyepokea msaada huo kwa ajili ya watoto wawili ambao ni
Linah na Joshua wanaosoma Shule ya Msingi Motomoto kata ya Ruiwa Wilaya ya
Mbarali Mkoani hapa alikishukuru chama cha Albino kwa msaada wa mafuta.
|
No comments:
Post a Comment