Wanachama wa bajajiwakiondoka mara baad ya kutoa msaada wa chakula kituoni hapo
Chama
Cha Waendesha Bajaji Jijini Mbeya, kupitia kwa mlezi wao, Mwaka Mwakisu wametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru Kilichopo Uyole
ambapo wametoa msaada wa vitu mbalimbali ambavyo ni vyakula vyenye thamani
ya shilingi 320,000.
Mlezi wa chama hicho cha
waendesha Bajaji, Mwaka Mwakisu, alitumia fursa hiyo kuwataka vijana na
jamii kwa ujumla kuwa na moyo wa huruma na kutojihusisha na matukio ya unyama
kama hayo ya kutupa watoto wasiokuwa na hatia.
“Kama tulivyosikiwa wenyewe
vijana hapa historia ya watoto hawa kutoka kwa mlezi wao, alivyosema kuwa tangu
kuanzishwa kwake kwa kituo hiki walianza na watoto wawili mwaka 2013 lakini leo
hii wamefikia idadi ya watoto 17 na kibaya zaidi mama huyu anasema watoto
wamekuwa wakiokotwa wakiwa wametupwa majalalani na kutelekezwa”
“Jamani hali hii inatia uchungu
kwa kweli watoto kama hawa hali waliyonayo ni lazima ifike mahala jamii
hususani akina dada kuwa na moyo wa huruma kuliko kuwa na moyo wa
kikatili kama huu” alisema Mwakisu.
Aidha, Mwakisu aliwataka vijana
na jamii kwa ujumla kuwa walinzi wa karibu kwa akina mama ambao wanaona wapo
katika hali ya ujauzito kuwachunga na kwamba pindi atakapoonekana kutokuwa na
ujauzito ni bora akaulizwa na kama hana mtoto achukuliwe hatua zaidi ili
kuweza kupunguza idadi ya watoto yatima.
Awali Mlezi watoto hao
katika kituo hicho, Rose Kawiche, alisema kuwa ongezeko la watoto wanaotupwa
limekuwa likiongeza siku hadi siku.
“Kwa kweli idadi ya watoto
imekuwa ikongzekeza siku hadi siku kwa mfano kwa mwaka jana pekee tumepokea
watoto watano na sasa ninawatoto 17, na hawa wote ni wale wamekuwa wakiokotwa
majalalani wakiwa bado kichanga na kwamba kama hawa mnaowaona hapa umri wao
hauzidi miezi sita na saba” mpaka miaka mitano alisema mama huyo huku akionekana kutokwa na
machozi.
|
1 comment:
Ni wakati wa watanzania wote kutumia nafasi zetu ktk kusaidia watoto yatima kama walivyofanya hiki chama cha bajaj kwanza nawapongeza sana kwa moyo huo na mungu awabariki sana.
Post a Comment