MNAMO
TAREHE 06.02.2013 MAJIRA SAA
00:30HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA
MWAMBANI – MKWAJUNI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA . ASKARI POLISI G.68 PC JAFARI KARUME MOHAMED MIAKA 30,MUHA
WA KITUO CHA POLISI MKWAJUNI
ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO .
CHANZO CHA TUKIO NI MAJAMBAZI
WANNE WAKIWA NA SILAHA
IDHANIWAYO KUWA AINA YA SMG WALIVAMIA KITUO CHA MAFUTA KILICHOPO KIJIJI
CHA MATUNDASI MALI YA SAMORA S/O MUYOMBE
NA KUPORA PESA TSHS 2,200,000/=
WAKITUMIA GARI T.227 BST AINA YA TOYOTA COROLA ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA SHABAN S/O MSULE,MIAKA 33,MBENA MKAZI
WA MAKAMBAKO .MAREHEMU AKIWA DORIA NA ASKARI WENZAKE WALIFUATILIA TUKIO HILO NA
KATIKA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI ASKARI HUYO ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA
RISASI UBAVU WA KULIA NA KUKIMBIZWA HOSPITALINI KWA MATIBABU ZAIDI . KATIKA
TUKIO HILO JAMBAZI SHABAN S/O MSULE
ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI .GARI
LILILOTUMIKA KATIKA TUKIO HILO LIMEKAMATWA NA MAGANDA 9 YA RISASI AINA
YA SMG/SAR NA RISASI 6 ZIMEOKOTWA ENEO LA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU ASKARI G.68 PC JAFARI KARUME MOHAMED
UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO .MSAKO MKALI UNAENDELEA CHINI YA UONGOZI WA RCO
MBEYA ROBERT MAYALA – SSP, ASKARI POLISI NA WANANCHI ILI KUWABAINI NA KUWAKAMATA WATUHUMIWA
WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI .KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU
MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI
ANATOA WITO KWA MTU/WATU WENYE
TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE , VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.
[ BARAKAEL MASAKI – SSP ]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment