Sarah
A. Mwaseba
Ndugu wanahabari, salaam!
Ndugu wanahabari, Kwanza hatunabudi
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ulinzi anaotupatia na uwezo wa kutambua fikra
zetu. Tunawashukuru viongozi wetu wa NCCR - Mageuzi kwa kututambua na kufika
Mbeya ili kutupokea.
Pia tunawashukuru waandishi wa habari
wote kwa kazi nzito inayowafanya muwe maadui na marafiki katika utekelezaji wa
majukumu yenu kwa Taifa letu. Mungu na awajalie ulinzi mkuu katika kutekeleza
majukumu yenu.
Ndugu Wanahabari,
Sisi ni sehemu tu tunaohamia
NCCR-Mageuzi kutoka CHADEMA na vyama vingine. Kimsingi tumetangulia na tumeamua
kujitokeza mbele ya watanzani kupitia kwenu wanahabari ili kuwa mashuhuda wa kisiasa.
Wapo wenzetu wanaohama kimya kimya
kimwili na kifikra. Lakini wapo wengine tuliowaacha huko kwenye matawi yetu
tunakwenda kuwapokea na kuanza nao kazi mpya katika Demokrasia ya kweli na
mfumo bora wa kiutawala ndani ya NCCR Mageuzi.
Wapendwa wanahabari, harakati zetu
zina historia tofauti katika siasa za nchi hii. Wapo ambao leo hii wanarudi
NCCR baada ya kuhama miaka kadhaa iliyopita.
Lakini wapo pia wanaotoka CCM
na CUF. Lengo letu ni kuitoa CCM madarakani na kujenga utawala wa sheria na
Demokrasia ya kweli ndani ya vyama vyetu.
Kwa furaha kubwa kabisa tunapenda
kuchukua fursa hii kuwatangazia wana Mbeya na umma wa Watanzania kwa kuvunja
ukimya na sasa tunatangza rasmi kujiunga na Chama Cha NCCR- Mageuzi (
National Convention For Construction and Reform- Mageuzi) na tunasema tena
kuwa, tumejiunga kwa hiari yetu kutokana na kuikimbia CHADEMA kwa mambo yake
ambayo kwa uchache tunayaeleza kama ifuatavyo:
·
Uongozi wa kitaifa umefeli kujenga demokrasia ya kweli ndani
ya chama kwa kukumbatia ufisadi wa kutumia vibaya ruzuku ya chama.
Chadema mikoani imebaki ni
kujichangisha fedha kwa kila tukio la ujenzi wa chama utadhani hakuna pesa za
ruzuku na michango ya wafadhili.
·
Uongozi mbovu wa Mhe; Mbowe na dk. Slaa kwa kushindwa
kusimamia katiba ya chama katika kutatua migogoro ya chama na kuishia kuwa na
mbinu ya kufukuza wanachama wema kwa majungu wanayoyajenga wenyewe.
·
A tukisema ukweli wa ouvu wao jamii haiwezi kuamini.
Wanajidanganya!!!! Hii ni ishara ya kufinyanga katiba na kutoiheshimu
dhana ya nguvu ya umma.
·
Chama kujaa utashi wa nguvu ya umma na kulazimisha
maandamano, migomo kwa vitu visivyo na ulazima.
Sisi hatuwezi kuamini pamoja na
watu walio na malengo ya kuleta fujo kitaifa kwa kisingizio cha kutafuta
ukombozi mpya wa taifa.
·
Hatua ya kuwafukuza fukuza viongozi bila kuwasilikiliza
hususani wa nyanda za juu kusini.
·
Dk. Slaa kulipwa mamilioni ya pesa kama mshahara wake na
posho lukuki amejikusanyia na watu anaowataka Makao Mkuu.
·
Akina mama Mbeya walihamasishwa kuwa tuwe tunampokea
mchumba wa Katibu mkuu slaa kama mke wa raisi kumbe ni mwanachama wa kawaida
anayetumia vibaya rasilimali za chama.
·
Uwezo mdogo wa kutekeleza ahadi alizoahidi mbunge wa mjini
‘joseph mbilinyi’ kwa wananchi wa mbeya. Ameacha kuufanya ubunge kuwa ni
taasisi nyeti ya umma na ameamua kuutumia kama jukwaa la muziki na ameonesha
Mbeya hatuna uwezo wa maendeleo ya pamoja.
Wakati wa kampeni aliahidi kujenga mabwawa ya samaki, bandari ya
nchi kavu, vifaa vya hospitalini, benki ya wana Mbeya, umoja wa akina mama,
vikundi vya ujasiliamali vya kijamii, kuinua wasanii wa mbeya, kulifanya jiji
la mbeya liwe mfano wa kuigwa Tanzania.
Pia aliahidi kutatua kero ya elimu
(shule za kata), usafi wa jiji, mpango mzuri wa masoko ndani ya jiji. Lakini
hadi leo hakuna anachofanya zaidi na hata bungeni na kupandikiza chuki za
kukataa kupokea Raisi wa nchi anapokuwa na ziara mkoa wa mbeya.
· Mbunge ameendelea kuchochea wanachama
asiowataka wafukuzwe nafasi za uongozi na anaowataka walindwe.
Aliwahi mwambia DK, Slaa kuwa akimtoa
mwenyekiti wa wilaya ya mbeya mjini basi, yeye anarudisha kadi; masikini bila
kujua mzee wa watu dk. Slaa akamsikiliza na akageuka mbogo kwenye kikao cha
ndani na kuamua kuwalinda waharifu wa siasa za Mbeya na kuwafukuza ambao ‘SUGU’
hawataki. Dk. Slaa alionesha uwezo mdogo wa kudadavua mambo ya maneno ya
majungu.
Tumechukua uamuzi huu mzito wa kuhama
chadema na kujiunga na NCCR-Mageuzi kwa kuwa NCCR kwa matendo kimeonekana kuwa
chama cha UTU na chenye misingi bora ya usawa, uheshimu wa haki za wanachama na
watanzania na chenye mshikamano wa kweli.
S/N
|
JINA MWANACHAMA
|
WADHIFA NDANI YA CDM
|
KATA/TAWI
|
1:
|
Moses Aliko Mwasubili (bulldozer)
|
Katibu mwenezi wa wilaya
|
Mbeya mjini
|
2:
|
Emmanuel Amani Mwangoka (Cash Money)
|
Mpambe wa mbunge/mwanachama
|
Mbeya mjini
|
3:
|
Magrethy John M ota
|
Mjumbe wa kamati tendaji
|
Kata ya Isyesye
|
4:
|
Hosea A. Mwangoje
|
Mjumbe kamati tendaji na MC Kampeni za mbunge – SUGU
|
Mbeya mjini
|
5:
|
Sarah A. Mwaseba
|
Mwenyekiti wa BAWACHA
|
Kata ya Isyesye
|
6:
|
Emmanuel Nehemiah Ngogo
|
Mwenyekiti
|
Tawi la Tawi
|
7:
|
William Swila
|
Katibu mstaafu wa Wazee
|
Mkoa wa mbeya
|
8:
|
Jonathani Mwakalinga
|
Katibu mwenezi wa Kata
|
Kalobe
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Kimepitia migogoro mingi na ya
kutisha lakini bado ni imara na hivyo ni vema watanzania wakajenga imani na
chama Komavu kuliko CHADEMA ya watu wachache na iliyo furika majungu na ukabila
pia haina ukomavu na uzoefu wa migogoro. Migogoro kidogo tu iliyopo wamepoteana
na bado wameandaa migogoro mingi ya uchaguzi wa ndani ya chama.
Imetolewa na sisi:
Majina ya wanaohama toka CHADEMA
kuingia NCCR - MAGEUZI.
1 comment:
ha ha ha ha ha!!
they better go sisimu, I dont think they have effect in politics
Post a Comment