WILAYA YA MBEYA MJINI - MAUAJI
MNAMO TAREHE 03.02.2013 MAJIRA YA
SAA 18:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. AMBOKILE S/O KIKWALE,MIAKA
16,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA ILEMI ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA
MATIBABU HOSPITALINI HAPO BAADA YA KUPIGWA KWA KUTUMIA FIMBO NGUMI NA MATEKE NA
MAMA YAKE MDOGO [MAMA WA KAMBO ]
BUPE W/O JOSEPH KIKWALE,KYUSA,MIAKA 32,MKULIMA MKAZI WA ILEMI MAJIRA YA SAA 17:00HRS .CHANZO NI
MTUHUMIWA KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA ANAMUIBIA PESA NYUMBANI KWAKE ENEO LA ISANGA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WATATUE MATATIZO YA KIFAMILIA KWA NJIA YA
MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA RUNGWE - AJALI YA GARI NA KUSABABISHA KIFO
MNAMO TAREHE 02.02.2013 MAJIRA YA
SAA 19:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LWANGWA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA.
IPYANA S/O SILWIMI,MIAKA 36,KYUSA ,DEREVA MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA ALIRUKA
KUTOKA KWENYE GARI T.482 AYB AINA YA ISUZU ALILOKUWA AKIENDESHA KISHA GARI HILO
KUMKANYAGA . MAREHEMU ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA KATIKA
HOSPITALI YA MISHENI ITETE KWA MATIBABU. CHANZO CHA AJALI NI GARI KUSHINDWA
KUPANDA MLIMA NA KURUDI NYUMA AMBAPO DEREVA ALIAMUA KURUKA NA GARI KUMKANYAGA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO
KWA MADEREVA KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA KUWA NA
TAHADHARI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA
KUJITOKEZA.
WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA
NA BHANGI.
MNAO TAREHE 03.02.2013 MAJIRA YA
SAA 11:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBANGALA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.
ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA FRENK S/O HAMISI,MIAKA
25,MKULIMA,MNYIHA,MKAZI WA KIJIJI CHA CHANG’OMBE AKIWA NA BHANGI KETE 44 SAWA
NA GRAM 220 . MTUHUMIWA NI MUUZAJI
NA MVUTAJI WA BHANGI.TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA FAIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment