TAMKO LA
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA KUHUSU UCHOCHEZI WA KIDINI
Kwanza kabisa tungependa kutoa pongezi
kwa Viongozi na Waumini wa Dini na Madhehebu mbalimbali hapo Mkoa Mbeya
kuendeleza utamaduni wetu wa kuishi na kushirikiana katika shughuli mbalimbali
za kijamii. Bila kuweka hisia za udini. Tunawashukuru kwa kuendelea
kuvumiliana. Pamoja na kuendelea katika hali hii, kumejitokeza viashiria
mbalimbali vyenye kuonyesha dalili za kumomonyoka kwa maadili, katika Mkoa
wetu.
2.
Kumejitokeza baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa
Wakuzitumia nyumba zetu
takatifu za Ibada kuhubiri mambo
ambayohayahusiani kabisa na mambo yanayohusu Mwenyezi Mungu na
mafundisho yake, kwa kuhubiri mambo ya siasa za chuki kwa dhamira ya
kupandikiza chukidhidi ya Serikali au dini na madhehebumengine. Baadhi yao
wamediriki kuyasema hayo hadharani kwenye miadhara yao au mikusanyiko ya
waumini wao.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaona hali
hii haina
afya njema kwa mustakabali wa amani na utulivu wa Mkoa
wetu na
Nchi kwa ujumla.
3.
Pamoja
na mahubiri hayo pia kumekuwepo nyaraka mbalimbali za kimaandishi za sauti
katika kanda, CD zenye kuhubiri chuki, uchochezi dhidi ya dini au dhehebu lingine.
Kumekuwepo na video katika kanda, CD au DVD zenye kuhubiri chuki, uchochezi,
dharau na kebehi dhidi ya dini nyingine au Serikali na baadhi ya kanda hizo
zimediriki kuhamasisha waumini wake vurugu na hata kuua jambo ambalo Kamti ya
Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaamini hakuna dini ya aina yoyote
dunianiinayohimiza waumini wote kutumia kwa jambo lolote lile.
4.
Baada
ya kutafakari, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya imeamua yafuatayo:- inapiga marufuku:
(i)
Kuuza,
kusambaza au kuonyesha, Kanda za sauti CD za sauti, Kanda
za Video, CD, DVD, nyaraka
na maandiko yoyte yenye uchochezi wa aina yoyote ile au kukashifu dini yeyote
katika Mkoa wa Mbeya.
(ii)
Chombo
chochote cha Habari kilichopo Mkoani Mbeya kiepuke
kuandika makala, kunakili au kurusha hewani hotuba, mahubiri au
kuonyesha video zenye kuchochea, kudharau, kuhubiri au kukashifu
dini
yoyote ile
5. Kamati ya
Ulinzi na Usalama Mkoa inawaasa viongozi wa dini
Mbalimbali kutohubiri siasa kwenye majumba ya Ibada kwani
kwa
kufanya hivyo watakuwa wanakiuka sheria za nchi.
Mtawagawa
waumini wenu kwa sababu waumini wanaelewa hayo si maagizo
ya
Mungu, na hayamo kwenye vitabu vitakatifu.
6. Waandishi
wa Habari epukeni kushabikia matamko ya Viongozi wa
Dini au
Siasa yenye kulenga kuleta mgawanyiko katika taifa hili kwa
Misingi ya
kidini au kisiasa kwa kisingizio cha Uhuru wa Habari,
kumbukeni
Amani Umoja na Mshikamano wa Mkoa na Taifa
utategemea
mchango wenu katika kushabikia au kukemea kauli hizo
bila kujali
zimetolewa na kiongozi gain.
Mwisho, Serikali itamchukulia hatua za
kisheria mtu yeyote atakayekwenda kinyume na haya, bila kujali itikadi yake,
dini yake au wadhifa wake. Wananchi wanaaswa kuzikabidhi nyaraka, kanda CD na
DVD kwa ofisi za Serikali ngazi ya Vijiji, kata Wilaya na Mkoa au kituo
chochote cha Polisi. Endapo watakabidhi kwa hiyari hawatachukuliwa hatua.
Imetolewa na:
MWENYEKITI
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA
|
No comments:
Post a Comment