OFISA KATIKA IDARA YA ELIMU SEKONDARI AKIONYESHA NAMNA YA
KUUNGANISHA MFUMO WA MAJI KWENYE MEZA YA MAABARA
HALMASHAURI ya wilaya Mbozi imekabidhi meza nne za maabara
inayotembea kwaajili ya mafunzo ya vitendo katika masomo ya Baiolojia, Kemia ,
Kilimo na Fizikia kwa shule nne za sekondari ikiwa ni sehemu ya hatua za
kukabili changamoto za matokeo mabaya ya shule za sekondari katika masomo ya
sayansi.
Afisa Elimu sekondari wilayani Mbozi bwana Isaack Mgaya, amesema
meza hizo zenye thamani ya shilingi Milion 24 zinatokana na msaada uliotolewa
na serikali mwezi juni wa kiasi hicho cha fedha kwaajili ya kuziwezesha shule
za sekondari kuwa na Maabara zinazohamishika.
Amesema hatua hiyo inaziwezesha shule Mbili za sekondari kwa
wilaya mpya ya Momba za Mkulwe na Nkangamo kuwa na maabara wakati kwa upande wa
wilaya ya Mbozi shule za sekondari za Msia na Lumbila pia zimenufaika.
Bwana Mgaya amesema Mobile Laboratory kama zinavyofahamika
zimebuniwa ili kuwezesha kukidhi mafunzo ya masomo ya sayansi kwa vitendo
katika shule za sekondari na Vyuo.
Aidha alifafanua kuwa matumizi yake yanawezesha madarasa hayo
kuhama hama kulingana na mahitaji na kwamba pia zinaweza kutumika chini ya
miti, ama maeneo yasiyo na mifumo ya umeme ama maji hivyo kurahisisha uelewa wa
wanafunzi kulingana na mazingira waliyopo
kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Wilaya ya
Mbozi bwana Levison Chilewa ambaye aliambatana na Kaimu mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Momba Bwana Juma Kitabuge ameeleza kuwa kutokana na
muundo wa maabara hizo, madiwani wa kata zilizonufaika na mpango huo wanapaswa
kujenga hoja za kushawishi madiwani wenzao ili kutenga kiwango kikubwa cha
fedha za mapato ya ndani ya halmashauri hizo mbili kwaajili ya ununuzi wa meza
hizo ambazo zitakuwa mkombozi kwa watoto katika masomo ya sayansi.
Alisema hivi sasa wanafunzi wamekuwa waoga wa masomo hayo
kutokana na mazingira ya kusomea kutokuwa yenye mvuto ikiwa ni pamoja na
kukosekana kwa zana muhimu na maabara, na kwamba hatua ya kusambazwa kwa
teknolojia hiyo rahisi kunawawezesha wanafunzi sasa kujifunza katika hali
iliyobora zaidi kwa vitendo.
Alisema ni vyema pia kwa shule zilizo karibu kuona namna ambavyo
zinaweza kushirikiana kutumia maabara moja kwa kutembeleana hatua ambayo
itarahisisha katika ufundishaji na hata kuleta tija katika matumizi ya maktaba
hizo badala ya kuazimisha meza hizo kutoka shule moja kwenda shule nyingine
hali ambayo inaweza kusababisha uharibifu.
Akizungumzia msaada huo, diwani wa kata ya Ruanda bwana Keneth
Mgala amesema, kimsingi hatua hiyo itasaidia kupunguza hali ya matokeo mabaya
kwenye masomo ya sayansi ambapo wanafunzi wakti mwingine wanalaumiwa kwa
kuonewa kutokana na mazingira yenyewe ya shule kukosa vitu muhimu kama maabara
hivyo kushindwa kuhamisha nadharia katika vitendo ama kuoanisha vyote viwili.
Kwa kipindi kirefu,Shule pekee yenye maabara ya kubuniwa na
utundu wa mwalimu mmoja wilaya ya Mbozi ipo katika shule ya sekondari ya Vwawa
ambapo maaabara hiyo imekuwa shule kadhaa zimekuwa zikitembelea na
kujifunza ubunifu huo kwa lengo la kwenda kutengeneza katika shule
zingine ili kuongeza hamasa ya wanafunzi kupenda masomo ya sayansi
Kwa hisani ya Danny Tweve wa Indaba blog.
|
No comments:
Post a Comment