Mamlaka
ya Uthibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na majini( Sumatra) Mkoani Mbeya imesitisha utoaji wa leseni ya kubeba abiria wa kawaida kwa waombaji wapya wenye
magari yenye uwezo wa kubeba abiria
wasio zidi 14.
Aidha Mamlaka hiyo imesema kuwa endapo
wamiliki hao wa magari hayo watahitaji kutoa huduma kwa jamii mamlaka hiyo itatoa leseni kwa ajili ya kubeba watalii tu .
auli hiyo
imetolewa leo jijini Mbeya na Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Ndugu Diwani
Athumani wakati akizungumza na madereva wa mabasi madogo yaendayo Mji mdogo wa
Tunduma Wilayani kufuatia kuwepo kwa
mgomo uliodumu kwa miezi 3 sasa
ambao umefanywa na madereva hao kwa kuto safirisa abiria waendao
Tunduma.
Mgomo huo wa madereva
hao umesababishwa na baadhi ya wamiliki wa magari madogo aina ya( Noah) ambayo
yamekuwa yakifanya shughuli ya kubeba abiria toka Mbeya hadi Tunduma hali iliyo
zua mgogoro mkubwa baina ya wamiliki wa gari hizo Ndogo pamoja na madereva wa
Costa ambao ndio wenye leseni za
kusafirisha abiria Toka Mbeya hadi Tunduma.
wali wakati akizungumzana
madereva hao Kamanda Diwani amewataka mara moja watu wanaofanya biashara hiyo
kuacha mara moja kwani sheria itachukua mkondo wake.
Amesema sababu
kubwa ya kusitisa huduma inayo tolewa na magari hayo madogo ni kuzuia majanga
ambayo yanaweza kutokea kwani gari hizo hazina madirisha makubwa pamoja na
milango yake kuwa midogo ambayo na haina milango ya dharura endapo kunaweza
kutokea tatizo lolote.
Kufuatia hali hiyo Kamanda Diwani amewataka
madereva costa ambao wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa muda mrefu kuachana na mgomo huo badala yake waendelee
kutoa huduma kwa wananchi kama
ilivyo kuwa awali.
|
No comments:
Post a Comment