WILAYA YA
MBARALI - WATUHUMIWA WAWILI WAKAMATWA KWA WIZI WA MALI INAYOSAFIRISHWA
[SHABA]
MNAMO TAREHE 07.01.2013 MAJIRA YA SAA 01:00HRS HUKO
ENEO LA IGAWA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE KATIKA MPAKA KATI YA MIKOA YA
MBEYA/NJOMBE WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. WATU WASIOFAHAMIKA WALIVUNJA BODI
YA GARI T.952 AMY/T.913 AMY AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIMEBEBA SHABA KUTOKA
NCHINI ZAMBIA KUELEKEA DSM NA
KUIBA SHABA AMBAYO IDADI NA THAMANI YAKE BADO HAIJAFAHAMIKA. KUFUATIA TUKIO HILO POLISI
WALIFANYA MSAKO MKALI NA TAREHE 08.01.2013 KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA
WAWILI 1. DAUD S/O WATSON, MIAKA
31,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA UBARUKU MBARALI NA 2. SIMON S/O KABASI,MIAKA 23,MMALILA,MKULIMA MKAZI WA UYOLE MBEYA
WAKIWA NA VIPANDE TISA [9] VYA SHABA
NA WALIPOHOJIWA WALIKIRI KUFANYA
UHALIFU HUO . MBINU ILIYOTUMIKA NI KUIBA SHABA HIYO NA KUJIFICHA PORINI UMBALI
WA KM 7 KUTOKA ENEO LA TUKIO WAKIWA NA VIELELEZO. WATUHUMIWA WAMEKAMATWA NA
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA PIA JITIHADA ZA KUWATAFUTA
WATUHUMIWA WENGINE WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA NA MAKAZI YAO AMBAO
WALIKIMBIA ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TAMAA YA KUJIPATIA MALI/KIPATO CHA HARAKA
KWA NJIA ZISIZO HALALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA RAI KWA
MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA WALIKO WATUHUMIWA WALIOKIMBIA AZIFIKISHE TAARIFA
HIZO POLISI MAPEMA ILI WAKAMATWE.
KUINGIA
NCHINI BILA KIBALI
MNAMO TAREHE 08/01/2013 MAJIRA YA SAA 19:00HRS HUKO
KASUMULU WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA ABEL S/O ABIY, 25YRS,
AKIWA NA WENZAKE ISHIRININ NA NNE [24] WOTE RAIA WA ETHIOPIA WAKIWA WEMENGIA
NCHINI BILA KIBALI. MBINU
ILIYOTUMIKA NI DORIA. WATUHUMIWA WAMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA
YA UHAMIAJI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KWA MAMLAKA HUSIKA JUU YA
MTU/WATU WASIOWAFAHAMU/WATILIA MASHAKA KATIKA MAZINGIRA YAO WAZITOE ILI
WAKAMATWE KWANI WENGINE SI WEMA
KWA USALAMA WA NCHI.
Signed By,
[ADAM .P. SIMFUKWE - SSP]
Kny: KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment