SIRAHA ZA JADI ZILIZOKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA
MNAMO TAREHE 28.01.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS MAAFISA WA HIFADHI YA MALIASILI
NA UTALII WAKIONGOZWA NA MENEJA WA HIFADHI HIYO KASMIR S/O NGOWI NA AFISA MISITU WA JIJI LYOWA S/O WAYANGA KWA KUSHIRIKIANA
NA ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA
WALIFIKA KATIKA MTAA WA ISENGO KATA YA IZIWA KWA AJILI YA KUENDELEA NA
OPERESHENI YAO YA KUWAONDOA WATU WALIOVAMIA NA KULIMA NDANI YA HIFADHI YA SAFU YA MLIMA MBEYA [MBEYA RANGE FOREST RESERVE] ENEO AMBALO NI CHANZO CHA MAJI
NA VIUMBE HAI ZOEZI LILILOANZA TANGU TAREHE 28.12.2012.
HATA HIVYO KABLA ZOEZI HILO KUANZA KUNDI KUBWA LA WANANCHI WA
ENEO HILO WAPATAO 400 WAKIWA NA
SILAHA ZA JADI WALIFIKA ENEO HILO
WAKIWA WAMEJIANDAA KUFANYA VURUGU
WAKISHINIKIZA KUTOFANYIKA KWA ZOEZI HILO. KATIKA VURUGU NDOGO ILIYOTOKEA YOHANA
S/O MDEWA,MIAKA 54,MSAFWA,MWANACHAMA WA ASASI YA KIRAIA YA KUTUNZA
MAZINGIRA MKAZI WA KIJIJI CHA
IHOMBE , ALIJERUHIWA KWA KUKATWA PANGA KICHWANI , WAKIDAI NDIYE MSALITI
ALIYEWALETA WATU HAO ,HIVYO POLISI WALIMUOKOA NA KUMHIFADHI KATIKA OFISI YA
MTENDAJI KATA.
PIA KATIKA VURUGU HIZO KULITOKEA UHARIBIFU KATIKA GARI STJ 1830 MALI YA WAKALA WA HIFADHI YA MISITU NYANDA ZA JUU KUSINI KWA KUPASUKA WIND SCREEN YA MBELE NA SIGHT
MIRROR YA KUSHOTO NA MAGARI
MENGINE YA IDARA HIYO STJ 1821 NA STJ 1832 KURUSHIWA MAWE PIA KUBOMOA MADARAJA MAWILI YALIYOPO KIJIJINI HAPO. KUFUATIA HALI HIYO KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA MKOA WA
MBEYA WALIFIKA ENEO HILO HATA
HIVYO WANANCHI WALITAWANYIKA KWA KUKIMBIA. POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA ENEO HILO WALITOA WITO KWA
WANANCHI KUTOJICHUKULIA SHERIA MKONONI AMBAPO WALIKIRI NA KUDAI
HAWAKUELEZWA JUU YA ZOEZI HILO NA WAMEAHIDI KUJENGA WAO WENYEWE MADARAJA WALIYOKUWA WAMEBOMOA.
UONGOZI WA SERIKALI YA WILAYA YA
MBEYA CHINI YA MKUU WA WILAYA DR NORMAN SIGALA NA MSTAHIKI MEYA WA JIJI ATHANAS KAPUNGA NA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIWEMO MHE DIWANI NA MTENDAJI KATA YA IZIWA KATIKA KIKAO
KILICHOFANYIKA BAADAE WAMEKUBALIANA KUWA WATU WOTE WALIOVAMIA ENEO HILO
WAHAKIKISHE WAMEHAMA KABLA YA MWEZI AGOST
– 2013. KWA SASA HALI IMEREJEA
KUWA SHWARI KIJIJINI HAPO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII
KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAHESHIMU
NA KUTII SHERIA PASIPO KUSHURUTISHWA. PIA ANAZIDI KUSISITIZA KUWA MAZUNGUMZO NDIO NJIA MUHIMU NA SAHIHI YA KUWASILISHA MALALAMIKO/KERO BADALA
YA FUJO NA VURUGU ZISIZOKUWA NA TIJA KWANI ZINAWEZA KULETA MADHARA NA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO YAO.
KAMANDA AMEAHIDI KUWA WALIOVUNJA SHERIA KWA KUMJERUHI YOHANA S/O MDEWA NA KUFANYA UHARIBIFU WA MADARAJA WATAFUATILIWA ILI
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment