Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, January 4, 2013

DK. HARRISON MWAKYEMBE ATEMBELEA UWANJA WA NDEGE SONGWE MBEYA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) Mhandisi Suleiman S. Suleiman akimwelezea Dk Harrison Mwakyembe jinsi uwanja wa ndege songwe unavyofanya kazi toka uzinduliwe mwezi wa 12 mwaka jana na kuwa sasa uwanja huo umebaki maendeo ya maegesho ya ndege kubwa kama boing 737 

Mmoja ya wahandisi wa ujenzi wa uwanja huo wa songwe akimwelezea waziri wa uchukuzi Dk Mwakyembe  akimwelezea hatuza za mwisho za ujenzi wa maegesho  ya ndege kubwa
Mkuu wa majeshi Tanzani Jenerali Mwamnyange akisalimiana na kuagana na RPC wa Mbeya Diwani katika kiwanja hicho cha songwe kabla ya kuanza kwa ziara ya waziri wa uchukuzi Dk Mwakyembe 
Jenerali Mwamnyange akiondoka uwanjani hapo kurejea Dsm alikuwepo Mbeya kwa mapumziko Mafupi
Huu ni mnara  wa kuongozea ndege katika kiwanja hicho cha Songwe Mbeya
Mwongoza ndege mwandamizi John Chambo akimwezea waziri Mwakyembe jinsi wananvyofanya kazi ya kuongoza ndege katika mnara huo
Mkuu wa kitengo cha hali ya hewa Issa Hamad akimwelezea waziri mwakyembe juu ya shughuli zoa za upimaji wa hali ya hewa uwanjani hapo na mkoa kwa ujumla kuwa 
Hili ndilo eneo la maegesho ya ndege kubwa aina ya boing 737 ambalo mwishoni mwamwezi huu wa kwanza litakamilika
Hili ni eneo la kutua ndege na kurukia  barabara hiyo ya ndege inaurefu wa zaidi ya kilometa 3.5 km
Hii ni sura ya mbele ya uwanja huo wa songwe Mbeya
Hili ni jengo la kikosi cha zimamoto uwanjani hapo
Hawa ni waandishi wa habari walioanza kuripoti ujenzi wa uwanja huo tangu unaanza kujengwa mpaka sasa kulia kabisa  Chales Mwakipesile Brand Nelson Felix Mwakyembe na Joseph Mwaisango inaelekea kuna kitu wanashangaa
Waziri wa uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake katika uwanja huo wa songwe amesema kuwa uwanja wa Songwe wa kimataifa ni kati ya viwanja vikubwa viwili kujengwa baada ya uhuru ukitanguliwa na uwanja wa Mkoa wa Kilimanjaro kwani viwanja vingine vimekuwa vikifanyiwa marekebisho Tumeanzisha historia mpya kwani dunia inafahamau kwa sasa kuna uwanja wa kimataiafa wa Songwe, upo wazi umekamilika na umeanza kutumika alisema
Picha na Mbeya yetu

No comments: