MAREHEMU JOSEPH MWASOKWA
MNAMO TAREHE 09/12/2012 MAJIRA YA SAA
06:30HRS HUKO MAENEO YA BLOCK - T JIJI NA MKOA WA MBEYA. JOSEPH S/O NELSON
MWASOKWA, MIAKA 78,KYUSA, AFISA USALAMA WA TAIFA MKOA WA MBEYA [MSTAAFU] NA
MKAZI WA BLOCK T . ALIGUNDULIWA KUUAWA NYUMBANI KWAKE KWA KUKATWA NA KITU
CHENYE MAKALI KINACHODHANIWA KUWA NI PANGA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA MAKUBWA SEHEMU ZA SHINGONI,
KICHWANI MABEGANI NA MKONO WA KUSHOTO. KATIKA TUKIO HILO HAKUNA
KITU CHOCHOTE CHA MAREHEMU KILICHOCHUKULIWA KWANI MAREHEMU ALIKUTWA NA PESA
TASLIMU TSHS 107,000/= DOLA 200 ZA KIMAREKANI NA SIMU MOJA YA MKONONI. MBINU
ILIYOTUMIKA NI KUMVIZIA WAKATI AKIINGIA KWENYE GETI LA NYUMBA YAKE. KWA MARA YA
MWISHO MAREHEMU ALIRUDI NYUMBANI NA JIRANI YAKE MAJIRA YA SAA 20:00HRS TOKA
SOWETO KUTAZAMA FAINALI YA MPIRA WA MIGUU KOMBE LA CHALLENGE KATI YA UGANDA NA
KENYA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MTU/WATU
WENYE TAARIFA JUU YA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA
ZINAZOHUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
No comments:
Post a Comment