Kazi kweli kweli watoto wakimwimbia wimbo wa kumtania sharifu kuwa kapakaziwa mtoto |
Kwakweli tulikuta watoto wa shule ya msingi Mbata wamechangamka sana na kutupokea vizuri |
Sharifu huyo katikati jamani sasa mwachieni tunashukuru kwa kutuletea tuongee nae |
Rafiki yetu sharifu tayari wenzake wamemwachia na anaanza kutupa kisa cha kuachiwa mtoto mchanga |
Upendo Mwakipunda mwalimu wa shule ya msingi mbata amekiri kutokea kwa tukio hilo kweli walimpokea mtoto huyo na kumpeleka kituo cha polisi |
Tukiwa na mtoto sharifu baada ya kuongeanae habari kamili ya tukio hili tutawaletea jumatatu mara baada ya kufuatilia polisi na hospitali ya rufaa Mbeya |
Kwa ujumla baada ya kumaliza maongezi tulianza kuona jinsi watoto wakiwa katika michezo mbalimbali shuleni hapo dogo katulia dirishani mwa darasa lake huku akipata embe kwa raha zake |
Wengine madirishani wengine wanachora ukuta ni furaha tu shuleni hapo |
Wa kuruka kamba haya wa kucheza mpira sawa |
Wanafunzi wakifurahia chandarua walichobuni shuleni hapo |
Wakifurahia kutembelewa shuleni kwao |
Picha na mbeya yetu |
No comments:
Post a Comment