DAKTARI wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa
Mbeya,Paul Kisabi (32), amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya,
akikabiliwa na mashitaka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi
100,000 kutoka kwa mgonjwa aliyefikishwa Hospitalini hapo baada ya kupata
ajali.
Hatua hiyo imekuja baada ya Taasisi ya kuzui na Kuipambana na rushwa
nchini takukuru, kumtia mbaroni daktari huyo juzi kwa tuhuma za kupokea rushwa
ya kiasi hicho cha fedha baada ya kumuwekea mtego.
Daktari huyo Kisabi
amepandishwa kizimbani majira ya saa 3:45 na kusomewa mashitaka hayo mbele
ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, Fransis Kishenyi, aliyepangiwa
kusikiliza kesi hiyo ambayo imeibua hisia kali kwa wananchi.
Katika kesi hiyo
namba 237 ya mwaka 2012, upande wa mashitaka uliongozwa na waendesha mashita
wawili wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU), Joseph
Mulebya na Nimrod Mafwele.
Waendesha mashitaka hao walidai kuwa Disemba 19
majira ya asubuhi akiwa katika sehemu yake ya kazi katika kitengo cha upasuaji,
mshitakiwa alitenda kosa la kwanza la kushawishi rushwa ya shilingi 200,000
kutoka kwa mgonjwa Meshack Brown, aliyefika hapo kwa lengo la kupatiwa
matibabu.
Walisema katika kosa la pili, siku hiyo majira ya saa nane mchana
akiwa katika baa moja iliyojulikana kwa jina la Victoria iliyopo Jijini hapa,
mshitakiwa alitenda kosa lingine la kupokea hongo ya shilingi 100,000, huku
akijua kuwa vitendo vyote hivyo ni kinyume na sheria.
Walisema kuwa kwa mujibu
wa sheria za taasisi hiyo, makosa yote yaliyotendwa na mshitakiwa yanaangukia
kwenye kifungu cha 15 ibara ya 1 (a) cha sheria ya kuzuia rushwa namba 11 ya
mwaka 2007.
Kabla kupangwa tarehe ya kutajwa tena kesi hiyo, Wakili wa
mshtakiwa huyo, Ladislaus Rwekaza,aliiomba mahakama impe dhamana mteja wake
akidai kuwa makosa yanayomkabili yanadhaminika.
Hakimu Kishenyi alikubaliana na
maombi ya Wakili Rwekaza kuwa mashtaka yote yanayomkabili mshtakiwa
yanadhaminika na kusema dhamana yake iko wazi.
Alimtaka mshtakiwa huyo kutimiza
masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini mali yenye thamani ya
Sh,500,000, na kwamba awe na utambulisho wa barua kutoka kwa kiongozi wa
serikali ya mtaa .
Hata hivyo mahakama ililazimika kuahirishwa kwa muda wa
dakika 20 ili kutoa nafasi kwa mdhamini wa mshitakiwa kuleta barua hiyo baada
ya kudai kuwa alikuwa ameisahau kwenye gari lililokuwa nje ya jengo la
mahakama.
Baada ya kupokea ombi hilo hakimu Kishenyi aliwahoji waendesha
mashitaka kama wameridhika na hoja, ambao kwa pamoja walikubali kwa maelezo
kuwa dhamana ni haki ya kisheria kwa mshitakiwa hivyo hawakuwa na pingamizi.
Mshitakiwa
aliweza kutimiza masharti ya dhamana hiyo na hivyo kuachiwa huru hadi januari 7
mwaka 2013 ambapo kesi hiyo itaendelea kusikilizwa katika mahakama hiyo.
Kwa
mujibu wa kumbukumbu za mahama hiyo, mshitakiwa huyo Daktari Kisabi ni mmoja wa
mashahidi wa kesi nyingine inayoendelea mahakamani hapo ya mtoto Anethi
anayedaiwa kuchomwa moto katika mkono wake, kufungiwa ndani na kulazimishwa
kula kinyesi chake na Shangazi yake.
59
Habari na moses picha Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment