Akina mama hao wakiwa na hasira kali walisikika wakisema tuachieni kidogo tumfunze adabu
MWANAMKE
anayetuhumiwa
kumtesa kumlisha kinyesi na kumchoma moto mtoto wa kaka yake
kumfungia ndani, amepandishwa kizimbani kwa mara ya
pili katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kujibu
shtaka
linalomkabili.
Mwendesha
mashtaka
wa Serikali, Achiles Mulisa ameileza Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina
Mkandala (24)
Mkazi
wa Majengo jijini humo alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa
na
nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto Aneth Gasto (4).
Mulisa
akisoma
mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Gilbert
Ndeuruo
amesema kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha
222(a)
sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2002.
Kutokana
na hali hiyo
mwendasha
mashitaka huyo ameileza mahakama kuwa kesi inayo mkabili mwanamke
huyo
ilihitaji mashahidi sita ambao ni Dactari aliye mfanyia upasuaji
mtoto
huyo
mwenyekiti wa Mtaa na barozi wake pamoja na Askari
mpelelezi
wa kesi hiyo na mtoto mwenye .
Amesema
teyari
mashahidi wanne kati ya sita wamekwisha toa ushahidi wao mahakani hapo .
Kutokana
na
kosa hilo mshtakiwa amekana shitaka hilo ambapo alirudishwa mahabusu hadi
Novemba
27 Mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Amesema
upande
wa Jamhuri unamashahidi wanne ambao watatu kati yao teyari wamekwsha toa
ushahidi
wao katika mahakama hiyo .
Amewataja
mashahidi
hao kuwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shuku Mwakanyamale, Daktari
anayemtibu
mhanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dr. Paul Kasubi na Habiba
Mwakanyamale .
Wengine
ni
Askari Polisi aliyepeleza kesi hiyo WP Pudensia na Mtoto mwenyewe ambao
wako tayari kufika mahakamani na kutoa
ushahidi
wao mbele ya mahakama.
Awali
mshatakiwqa
huyo aliieleza mahakama kuwa na uhusiano na mtoto huyo ambapo
pia
alikiri kuwa na taarifa za kile kinachoendelea juu ya matibabu ya mtoto huyo
na
kuhusu kukatwa kwa mkono wake wa kushoto na kufungwa bandeji ngumu(POP)
kwenye
mkono uliobaki.
|
No comments:
Post a Comment