Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, November 26, 2012

LOWASSA AWAVAA WANASIASA NI KUHUSU VIJANA WA KIKE.

Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini Magharibi Alinikisa Cheyo akipokea mchango wa shilingi milioni 25 toka kwa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kike katika chuo kikuu teku 
Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini Magharibi Alinikisa Cheyo mara baada ya kupokea mchango huo akimshukuru waziri mkuu mstaafu Lowasa kwa kushiriki na kutoa mchango wake katika harambee hiyo
Kabla ya kuanza harambee hiyo,  waziri mkuu mstaafu  Lowassa aliongoza kuimba wimbo wa ‘’Bwana Mungu nashangaa kabisa’’ ambao mara kadhaa amekuwa akiuimba na kueleza kuwa anafarijika akiusikia na kuuimba wimbo huo wa tenzi za rohoni.


Kwaya ya Vijana Moravian Mbeya mjini wakiimba wimbo maalumu wa kumkaribisha waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa katika harambee hiyo


Mara baada ya kumaliza harambee hiyo mweshimiwa Lowasa akisalimiana na ndugu zake wamasai waishio Mbeya
Mweshimiwa Lowasa akiagana na kumpongeza MC  Chales Mwakipesile kwa kuongoza vizuri katika harambee hiyo


WAZIRI Mkuu Mstaafu , Edward Lowassa, amesema unyonge wa elimu kwa watoto wa kike hautamalizwa kwa kelele za wanasiasa , bali ni kwa taifa kuweka misingi imara itayowasaidia kujielimisha kadili ya ukomo wao, ili wawe na uwezo wa kutosha wa kupambana na changamoto zinazowakabili.

Kauli hiyo aliitoa jana Jijini hapa, wakati akiendesha harambe ya kuchangia ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU),kinachomilikiwa na kanisa la MoravianiTanzania (KMT) na kufanyika katika usharika wa Ruanda jimbo la kusini Magharibi.

Katika harambe hiyo Lowassa alichangia fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 25, huku viongozi mbalimbali wa serikali na chama tawala (CCM) wakiongozwa na na Mkuu wea Mkoa wa Mbeya,Abas Kandoro aliyewakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispine Meela nao wakitoa mchango wao.

Lowasa alisema ili taifa liweze kujidhatiti kikamilifu ni lazima watu wake wakaona fursa na kuamua kuwekeza kwenye elimu , ambapo kundi kubwa la vijana wataweza kujifunza na kuelimika katika mambo mbalimbali.
Alisema jitihada za kuwakomboa wanawake hususani watoto wa kike haziishi tu kwa viongozi wa siasa kupiga kelele majukwaani, bali ni watanzania kuwajengea uwezo wa kila hali ili kuhakikisha wanasoma kwa kadili ya ukomo wao.

Akizungumzia vijana kwa ujumla Lowassa alisema wanapaswa kutambua kuwa elimu ndio njia pekee ya wao kujikatika changamoto mbalimbali, hivyo bila nyenzo hiyo hawawezi kufika mahala popote, badala yake fursa mbalimbali zitawapita na wao kubaki watazamaji.
“Baba Askofu kwani hata ukitaka kufuga kisasa au kibiashara lazima uwe na elimu, na hata wale waliojiandaa kufanya kazi za ofisini wanakuwa na hali ngumu bila kuwa na elimu ya kutosha” alifafanua Lowassa.
Aliwata vijana kutumia vizuri fursa walizopata za kusoma katika vyuo vikuu iwe kwa ufadhili wa watu au serikali kwani watu hao waliowafadhili walijinyima kwa malengo ya kuhakikisha wanawatimizia matakwa yao ambayo ni faida kwa taifa pia.

Hata hivyo alisema kama vijana wa Tanzania hawataelimika vya kutosha katika elimu ya juu hawataweza kutoa ushindani wa kutosha kwa wenzao kwenye soko la ajira kwa nchi za zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alinikuu kifungu cha Biblia “ Tumeambiwa katika bibilia takatifu…tusipojibiidisha kutafuta maarifa tutaishia kuwa wateka maji, wakata kuni kwa wenzenu (Joshua 9:21), kwa hiyo nalipongeza kanisa la Moraviani kwa bidii na umoja wao kwa kujenga chuo kikuu.”

Aidha, Lowassa aliweka wazi kuwa tabia yake ya kuchangia katika makanisa ni wito na kamwe yeye si tajiri bali amekuwa ana changiwa na baadhi ya marafiki zake wanaoshirikiana hivyo kupata fedha hizo ambazo anazitoa kwenye harambe m,balimbali anazoombwa kuendesha na kuchangia.

“Mimi naenda sana kwenye harambe sijafirisika, lakini mimi sio tajiri kama watu wanavyosema ila huwa nachangiwa na wenzangu na hivyo kuwa na nguvu ya kuchangia kwenye makanisa kama mtakavyoona leo” alisema Lowassa.

Hata hivyo Lowassa alilipongeza kanisa hilo kwa utulivu kwa kusema ni tofauti na miaka iliyopita kwa kanisa hilo kuandamwa na migogoro mingi ambayo ilisababisha kanisa kukosa utulivu na kuwayumbisha waumini wake.

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa kanisa hilo Jimbo la Kusini Magharibi, Alinikisa Cheyo, katika harambee hiyo lilitarajia kukusanya kiasi cha shilingi milioni 500 ili kuweza kumalizia ujenzi wa mabweni kwea wanafunzi wa kike katika chuo hicho.

Na Moses Ng’wat,Mbeya. picha na mbeya yetu

No comments: