UBOVU wa bara bara katika Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya umesababisha hali za maisha za wananchi wa wilaya hiyo kuendelea kuwa duni kutokana na kushindwa kusafilisha mazao wanayolima kwenda mikoa mingine.
Akizungumza na mwandishi Esthar Macha wa mtandao huu ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bi.Rosemary Senyamule alisema hayo kufuatia ubovu huo wa bara bara ambao umedumu kwa muda mrefu bila jitihada zozote za kuhakikisha kuwa zinatengenezwa ili wananchi waweze kuwa na hali nzuri za kimaisha.
Alisema kuwa ubovu huo wa bara bara umekuwa ni tatizo kubwa kwa wananchi na hata kushindwa kushindwa kusafilisha mazao na vitu vingine ambavyo ni mkombozi kwa wananchi ambavyo vingeweza kuokoa hali za maisha.
“Hili suala la miundo mbinu katika wilaya hii ni tatizo kubwa sana ambalo linasababisha uchumi wa wananchi wa wilaya hii kuendelea duni ,ili kuweza kufanikisha hili serikali inaendelea kufanya jitihada ili kuhakikisha kuwa miundo mbinu hii inatengenezwa mapema”alisema.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema hilo likifanikisha hali ya uchumi kwa wananchi itaweza kubadilika haraka na wanancghi kuweza kufanya kazi zao kwa mara moja ,hivi sasa safari ya kutoka Mpemba Ileje mwananchi anatumia masaa matatu mpaka manne wakati ni safari ya saa moja tu.
Aidha Bi.Senyamule alisema kama serikali wanaendelea na na jitihada aza kuhakikisha kuwa bara bara hiyo inatengenezwa na kupewa kipaumbele kwenye bajeti ijayo .
Mmoja wa wananchi wa Tarafa ya Kipambawe Wilayani hapa Bw.Sifanuel Luka alisema kuwa tatizo la kutokuwa na bara bara nzuri katika wilaya hiyo limekuwa ni shida kubwa kwao kwa kushindwa kusafirisha vitu muhimu kwao ambavyo vingeweza kuondoa ugumu wa maisha.
“Kwa ujumla hili ni tatizo kubwa sana sehemu ya kwenda na kurudi inakulazimu mpaka ulale kwa hali hii maisha lazima yawe magumu kwa sisi wananchi,wilaya hii ni muda mrefu hebu angalia maisha ya wananchi wa wilaya hii walivyo na maisha magumu serikali ifanye jitihada mapema kuhakikisha kuwa bara bara hii inatengenezwa haraka”alisema.
No comments:
Post a Comment