VIONGOZI wa kata na vijiji
nchini wameshauriwa kuwa kipaumbele kusaidia wizara ya afya na ustawi wa
jamii kwa kutoa elimu kupitia mikutano ya adhara kwa jamii hususan
wakinamama wajawazito kuondokana na dhana ya kujifungulia majumbani au
kwa wakunga wa jadi ili kuondokana na changamoto hiyo inayochangiwa na
uelewa mdogo wa kushiriki katika vituo vya afya na zahanati hususan vijijini.
Akizungumza na waandishi
wa habari hivi karibuni Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Prisca Butuyuyu
alipokuwa akizungumzia mikakati ya wizara kukabiliana na changamoto ya
kupunguza tatizo hilo ili kufikia malengo ya sekta ya uzazi na mtoto
kupata takwimu sahihi za wakinamaa wanaoshiriki katika vituo vya afya na
zahanati.
Alisema katika kukabiliana
na hilo wizara ya afya inamikakati kabambe ya kuhakikisha
kuwa elimu hiyo inatolewa vijijini ambapo ndio kuna changamoto kubwa ya
mwamko duni ya wakinamama wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya
na zahanati.
|Alisema kuwa utafiti
uliofanywa umegundua changamoto hiyo inachangiwa na kuwepo kwa
uhaba wa vyombo vya usafiri ubovu wa miundombinu na umbali wa
vituo vya afya na kwamba serikali kupitia wizara ya afya inatakiwa
kufanya jitihada za haraka kusogeza huduma za afya vijijini ili kunusuru
vifo vya wakinamama wajawazito wakati wa kujifungua.
":Hii ni changamoto
kubwa kwa serikali na kwamba mikakati inatakiwa kuwepo ikiwa ni pamoja na kutoa
elimu ya kutosha kwa jamii kutambua umuhimu wa kujifungulia katika vituo vya
afya na zahanati ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza
wakati wa kujifungua ikiwa ni pamoja na kupatiwa kinga za kuzuia maradhi kutoka
kwa mama kwenda kwa mtoto"Alisema.
"Kwa kweli
ushirikishwaji wa utoaji elimu kwa jamii wahitajika kwani kila kukicha idadi na
takwimu zinazidi kuongezeka na hivyo ni jukumu la viongozi wa vijiji na mitaa
kutoa elimu kwa jamii kupitia mikutano ya adhara ili kusaidia na serikali
kupiga vita changamoto hiyo "Alisema.
Aidha alifafanua kuwa
takwimu za mkoa wa mbeya katika kipindi cha mwaka 2011 kwa wilaya ya
Ileje ndio inayoongoza kwa tatizo hilo kutokana na kuwa na idadi ndogo wa akina
mama wanaojifungulia kwenye vituo vya afya.
Alisema katika
wilaya ya Ileje ni asilimia 33 tu ya akina mama wajawazito walijifungulia
kwenye vituo ambapo asilimia 57 walijifungulia majumbani huku wilaya ya mbeya
mjini ndio ambayo ina idadi kubwa ya akina mama wanaojifungulia kwenye vituo
ambapo asilimia 109 ya akina mama wajawazito walijifungua kwenye vituo vya afya
.
Na Hawa Mathias,Mbeya.
|
No comments:
Post a Comment