Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, September 27, 2012

Kushuka kwa uwajibikaji na utendaji kazi wa watumishi wa idara mbalimbali hapa nchini kunatokana na mfumo mbovu wa elimu ya sasa hapa nchini.

Maggid Mjengwa mkufunzi mafuna ya online journalism

Baadhi ya washiriki wasemina wakimsikiliza kwa makini mkufunzi


picha ya pamoja



Waandishi wa habari mkoani Mbeya wamesema kushukwa kwa uwajibikaji na utendaji kazi wa watumishi wa idara mbalimbali hapa nchini kunatokana na mfumo mbovu wa elimu ya sasa hapa nchini.

wameyasema hayo katika  mafunzo ya uandishi wa habari kwa njia za mtandao ambayo yameandaliwa na umoja wa klabu za wa andishi wa nchini  (UTPC( na kufanyika katika ukumbi wa hospitali ya mkoa Mbeya.

wamesema watendaji wa idara mbalimbali wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi kutokana na kukoskana kwa uzoefu, ujuzi na elimu kwa wakati mmoja.
kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo MAGGID MJENGWA amesema mfumo wa Serikali kuangalia zaidi elimu pasipo Ujuzi na uzoefu wa mazingira umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa kutufika hapa tulipo.

Aidha amesema viongozi wa sasa wamekuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na kutojitambua, kujiamini na kuthubutu ikwia ni pamoja na kufanya kazi zao kwa shinikizo la usiasa badala ya kuangalia namna ya kutumia jamii.

No comments: