Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, September 29, 2012

VIONGOZI wa kata na vijiji nchini wameshauriwa kuwa kipaumbele kusaidia wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa kutoa elimu kupitia mikutano ya adhara kwa jamii



VIONGOZI wa kata na vijiji nchini wameshauriwa kuwa kipaumbele kusaidia  wizara ya afya na ustawi wa jamii  kwa kutoa elimu  kupitia mikutano ya adhara kwa jamii hususan wakinamama wajawazito  kuondokana na dhana ya kujifungulia majumbani au kwa wakunga wa jadi ili kuondokana  na changamoto hiyo inayochangiwa na uelewa mdogo wa kushiriki katika vituo vya afya na zahanati hususan vijijini.




Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni Mratibu wa afya  ya uzazi na mtoto Prisca Butuyuyu alipokuwa akizungumzia mikakati ya wizara kukabiliana na changamoto ya kupunguza  tatizo hilo ili kufikia malengo ya sekta ya uzazi na mtoto kupata takwimu sahihi za wakinamaa wanaoshiriki katika vituo vya afya na zahanati.


Alisema katika kukabiliana na hilo  wizara ya afya inamikakati kabambe  ya kuhakikisha  kuwa elimu hiyo inatolewa vijijini ambapo ndio kuna changamoto kubwa ya mwamko duni ya wakinamama wajawazito  kujifungulia katika vituo vya afya na zahanati.




|Alisema kuwa utafiti uliofanywa umegundua  changamoto hiyo   inachangiwa na kuwepo kwa uhaba wa vyombo vya usafiri  ubovu wa miundombinu  na umbali  wa vituo vya afya na kwamba  serikali kupitia wizara ya afya inatakiwa kufanya jitihada za haraka kusogeza   huduma za afya vijijini ili kunusuru vifo vya wakinamama wajawazito wakati wa kujifungua.

":Hii ni changamoto kubwa kwa serikali na kwamba mikakati inatakiwa kuwepo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa jamii kutambua umuhimu wa kujifungulia katika vituo vya afya na zahanati ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza wakati wa kujifungua ikiwa ni pamoja na kupatiwa kinga za kuzuia maradhi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto"Alisema.


"Kwa kweli ushirikishwaji wa utoaji elimu kwa jamii wahitajika kwani kila kukicha idadi na takwimu zinazidi kuongezeka na hivyo ni jukumu la viongozi wa vijiji na mitaa kutoa elimu kwa jamii kupitia mikutano ya adhara ili kusaidia na serikali kupiga vita changamoto hiyo "Alisema.




Aidha alifafanua kuwa  takwimu za mkoa wa mbeya katika kipindi cha mwaka 2011 kwa wilaya ya Ileje ndio inayoongoza kwa tatizo hilo kutokana na kuwa na idadi ndogo wa akina mama wanaojifungulia kwenye vituo vya afya.

 Alisema katika wilaya ya Ileje ni asilimia 33 tu ya akina mama wajawazito walijifungulia kwenye vituo ambapo asilimia 57 walijifungulia majumbani huku wilaya ya mbeya mjini ndio ambayo ina idadi kubwa ya akina mama wanaojifungulia kwenye vituo ambapo asilimia 109 ya akina mama wajawazito walijifungua kwenye vituo vya afya .

Na Hawa Mathias,Mbeya.

No comments: