SHIRIKA la VECO limesema kuwa litashirikiana na wakulima wa zao la Alizeti katika wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya na tayari limeanzisha mpango wa ujenzi wa majengo yatakayotumika kwa kwa lengo la kuboresha soko la mazao yao.
VECO limesema kuwa limetoa vifaa na gharama za ujenzi ambao una lenga kujenga majengo katika kata za Matundasi,makongorosi,Kanga(tete),Chalangwa na Sangambi na kuwa maeneo mengine ni Matanila na Ifumbo.
Alisema lengo la mpango huo wa kuhimiza kilimo cha alizeti ambao upo katika hatua ya pili una lenga kuboresha maisha ya wakazi wa wilaya hiyo, ili waweze kujiongezea kipato kutokana na kuuza bidhaa zao pamoja na kuwawezesha kuhifadhi mazao ya chakula.
Aidha Majaliwa alisema katika awamu ya kwanza iliyoanza mwaka 2004-2005 iliwezesha kuwahamasisha wakulima wa zao hilo kutoka wakulima 200 hadi 1600 ambao ni sawa na asilimia 70,ambao walikuwa ni wanawake na kuwa katika awamu ya pili ya mwaka 2009 -2014 shirika hilo lina mapango wa kuhakikisha linavuka malengo yake kwa kiwango kikubwa ili kuwaondolea wananchi hali ya umasikini.
Majaliwa alibainisha kuwa kuna idadi kubwa ya wakulima wa wilaya hiyo wanaoishi katika hali ya umasikini mkubwa, kutokana na wakulima wanache kutegemea zao la tumbaaku na kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa na ukataji miti ovyo.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa zao hilo wamepongeza uamuzi wa shirika la VECO kwa kuamua kuimarisha zao hilo wilayani Chunya, kwa kuwa litawawezesha wakulima wengi kujiimarisha kiuchumi kutokana na kuishi katika hali ya umasikini kwa muda mrefu kutokana na kutegemea zaidi zao la Tumbaku kwa muda mrefu.
Mmoja wa wakulima hao Frank Kavinga alisema tangu kuanzishwa kilimo cha alizeti wilayani humo na kisha shirika la VECO kuanzisha mpango wa kuliendeleza zao hilo, kumekuwa na mwamko wa wakulima wengi kulima alizeti badala ya zao la Tumbaku.
Alisema wengi wa wakulima wamekuwa wakipewa elimu ya mara kwa mara kuhusiana na faida za kilimo cha alizeti na kuwa VECO imekuwa msitari wa mbele kuwagawia wakulima mbegu za bure za zao hilo kwa lengo la kuharakisha kasi ya kilimo hicho.
Uamuzi wa mpango huo wa ujenzi wa majengo katika kata saba za wilaya hiyo ya Chunya unalenga kuwawezesha wakulima kukusanya na kuzalisha mazao ya alizeti kwa pamoja na kuweza kuyauza kwa faida.
Kwahisani ya Kalulunga
No comments:
Post a Comment