Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, September 14, 2012

CCM MBARALI WATISHIA KUSUSIA UCHAGUZI


BAADHI ya wanachama wa (CCM) Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wametishia kususua mkutano wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba 26, Mwaka huu kwa kilichodaiwa kujaa kwa mizengwe.

Wanachama hao ambao hawakutaka majina yao yaandikwe walisema wako tayari kuvuruga mkutano huo wa uchaguzi baada ya kusikia kuwa kuna majina ya baadhi ya wagombea hayatarudishwa kwa ajili ya kupigiwa kura.

Walisema  ili chama kisonge mbele ni lazima uchaguzi wa demokrasia ufanyike na si wanavyotaka baadhi ya viongozi ambao wanashinikiza kundi Fulani kuchaguliwa na si kwa maslahi ya chama na wanachama wenyewe.

Kufuatia uwepo wa uvumi huo wanachama hao wameiomba mamlaka inayohusika kutochuja jina la mgombvea yeyeto ili wajitokeze mbela ya mkutano kwa ajili ya kuomba kura kwa wanachama na siyo kuondolewa kutokana na matakwa ya mtu au watu wachache.


Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Mbarali Paul Mwita  alikanusha kuwepo kwa harakati hizo ambapo alisema ni hali ya kawaida katika harakati za uchaguzi  hivyo wanachama wanatakiwa kuheshimu taratibu za chama na si kufanya vinginevyo.

Aidha aliwatupia lawama vyama vya upinzani kuwa ndiyo wanaowapanga wanachama hao ili wavuruge uchaguzi ambapo alisema kila mwanachama wa CCM anayohakli ya kuchagua na kuchaguliwa kwa mujibu wa kanuni za chama.

Pia aliwasihi wanachama kuwapuuza wale wanapandikiza chuki miongoni mwao ambapo alisema tetesi hizop yeye hazijamfikia ofisini kwake na kuongeza kuwa endapo zitamfikia atazifanyia kazxi kutokana  na michakato ya uchaguzi kuendelea.

“ Mimi kama mkurugenzi wa uchaguzi sijapata malalamiko hayo lakini kama yapo basi ni uzushi na propaganda zinazoletwa na wapinzani kwa lengo la kutuvuruga lakini tumejiandaa vizuri na wanachama wanazijua taratibu na kanuni za chama hivyo nawasihi wasiwe na wasiwasi.” Alisema Mwita.

Katibu huyo alisema tarehe ambayo mkutano huo utafanyika ni Septemba 26, Mwaka huu ambapo nafasi zitakazofanyoiwa uchaguzi aliziutaja kuwa ni nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya, Mjumbe wa Nec, Wajumbe wa Mkutano mkuu wa Mkoa na wajumbe wa Mkutano mkuu wa Taifa.

Alizitaja nafasi zingine kuwa ni Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya na nafasi ya katibu Mwenezi wa Wilaya.

Aidha aliwataja wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya kuwa ni Ignasi Mgao, Hashimu Mwalyawa , Mathayo Mwangomo, Lucy Ngimba na Benedikti Masuva.

No comments: