NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo amekemea vikali tabia ya baadhi ya Wakuu wa Vyuo na walimu kufanya udahili wa wanafunzi katika vyuo vya Ualimu kote nchini kinyume cha taratibu za Wizara ya elimu.
Alisema taratibu za usajili wa wanafunzi wanaotakiwa kuanza masomo katika vyuo hivyo hutolewa na Wizara kwa kila chuo kupatiwa nakala ya majina ya wanafanzi wenye sifa za kujiunga na vyuo hivyo vya ualimu pamoja na majina mengine kupelekwa kwenye mitandano ya Intanet ili kuwepo na uwazi juu ya suala hilo.
Kauli hiyo aliitoa juzi mara baada ya kufanya ziara ya ghafla katika vyuo viwili vya ualimu vya serikali vya Mpuguso na Tukuyu vilivyopo Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa lengo kutambua uwepo wa wanafunzi waliosajiliwa kinyume cha utaratibu.
Aidha katika ziara hiyo Mulugo alibaini wanafunzi 147 kati ya 1039 waliosajiliwa na vyuo hivyo viwili bila kufuata utaraibu wa wizara ambao wote wapo mwaka wa pili wa masomo kwa ngazi ya Diploma na Ngazi ya Cheti..
Wanafunzi 27 walikutwa katika chuo cha Ualimu cha Tukuyu ambapo Chuo cha Ualimu Mpuguso walikua ni wanafunzi 120 ambao baada ya kubanwa kuhusu njia walioitumia kujiunga na vyuo hivyo baadhi yao walikiri kutoa rushwa huku wengine wakisingizia ndugu zao kufahamiana na wafanyakazi wa Wizara.
Hata hivyo kufuatia zoezi hilo Naibu Waziri aliamua kuwasamehe wanafunzi hao ili waendelee na masomo kutokana na wao kujitokeza na kumweleza ukweli juu ya namna na njia waliyoitumia kujiunga na vyuo hivyo licha ya kukosa sifa kutoka Wizarani.
Alisema suala hilo limekuwa likichafua Wizara pamoja na serikali kwa ujumla kwani wengi wao wamekuwa wakipokea rushwa ya kutoka kwa wazazi au wanafunzi ili wapate usajili huo .
Alisema hali hiyo pia imechangia kwa asilimia kubwa kuporomoka kwa elimu nchini kwani wengi wao wamekuwa wakimaliza masomo hayo na kuajiliwa na serikali huku wakiwa hawana sifa pamoja na kutokuwa na uwezo wa kufundisha.
Aliesema kila mwaka idadi ya ufaulu imekuwa ikishuka kutokana na kuwepo kwa walimu wengi wasio na uwezo wa kufundisha wanafuzi mara wanapo ajiliwa na serikali.
Aliongeza kuwa kumekuwepo pia na mazoea kwa wakuu wa vyuo hivyo mara baada ya kupewa nafasi na serikali kutumia nafasi hiyo kujinufasha wenyewe na kufanya vyuo hivyo kuwa kama vyao binafsi badala kusimamia elimu.
Kutokana na hali hiyo Mulugo amewataka wakuu wote wa vyuo vya ualimu vya serikali kufuata taratibu za usajili kama magizo ya Wizara husika inavyo wataka vinginevyo hato sita kumchulia sheria mkuu yoyote wa chuo atakae kiuka taraitubu hizo.
Alisema mpango huo wa kukagua majina ya wanafunzi waliosajiliwa na Wizara utaaendela nchi nzima ili kubaini wale wote watakao kwenda kinyume na maagizo hayo ya wizara.
Katika hatua nyingine Naibu waziri huyo amebaini kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika chuo cha ualimu Mpuguso kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi waliosajiliwa kinyume cha taratibu za wizara inavyo agiza katika chuo hicho huku wakiwa hawana sifa pamoja na wengine kugundulika kutoa kiasi cha shilingi laki 3 na laki 4 ili wapate usajili katika chuo hicho.
Kwa hisani ya Venance Matinya, Rungwe.
|
1 comment:
Kweli Tanzania kuna ombwe la uongozi. Unafuatilia uozo halafu unagundua chanzo chake ni ofisi yako halafu unaishia kujifanya unasamehe.
Wamekwambia wametoa rushwa halafu unasema unasamehe wakati hao ni wahalifu.
Ndio hata polisi wanaua tu watu hata wasio na hatia wakijua hakuna watakachofanyiwa kwa maauaji ya raia.
Post a Comment