Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, September 30, 2012

MARUFUKU KUNUNUA UFUTA BILA KUFUATA TARATIBU ZA HALMASHAURI YA CHUNYA MBEYA

Mkuu wa wilaya ya Chunya Mheshimiwa Deodatus Kinawiro.

WAFANYABIASHARA wanaofanya biashara za ununuzi wa mazao wilayani Chunya Mkoani Mbeya wamepigwa marufuku kununua zao la ufuta bila kufuata taratibu za halimashauri hiyo.


Marufuku hiyo imetolewa juzi na Mkuu wa wilaya hiyo Deodatus Kinawiro katika kikao cha  baraza la madiwani. Alisema kwa muda mrefu sasa wakulima wengi wa zao la ufuta katika wilaya hiyo wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya udanganyifu na wafanyabiasha hao kwa kufanya ununuzi wa zao hilo kwa bei isiyo halali.

''Wafanyabiashara hao wanawaraghai wakulima hao kwa kununua zao hilo bila kufuata taratibu za upimaji  badala yake wamekuwa wakitumia ndoo hali inayo fanya mkulima huyo kuendelea kuumizwa'' alisema Mkuu wa wilaya huyo.

Amesema serikali haipigi marufuku ununuzi huo ili kumumiza mkulima bali inafanya hivyo ili kuinua pato la mkulima kwa kuhakikisha anapata bei nzuri inayo mnufaisha.

Sanjari na hayo amepiga marufuku wafanyabiashara kuwakopesha wakulima fedha kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa kilimo.

No comments: