picha ya pamoja
Waandishi wa habari mkoani Mbeya wamesema kushukwa kwa
uwajibikaji na utendaji kazi wa watumishi wa idara mbalimbali hapa nchini
kunatokana na mfumo mbovu wa elimu ya sasa hapa nchini.
wameyasema hayo katika
mafunzo ya uandishi wa habari kwa njia za mtandao ambayo yameandaliwa na
umoja wa klabu za wa andishi wa nchini
(UTPC( na kufanyika katika ukumbi wa hospitali ya mkoa Mbeya.
wamesema watendaji wa idara mbalimbali wamekuwa wakishindwa
kufanya kazi zao kwa ufanisi kutokana na kukoskana kwa uzoefu, ujuzi na elimu
kwa wakati mmoja.
kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo MAGGID MJENGWA
amesema mfumo wa Serikali kuangalia zaidi elimu pasipo Ujuzi na uzoefu wa
mazingira umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa kutufika hapa tulipo.
Aidha amesema viongozi wa sasa wamekuwa wakishindwa
kutekeleza majukumu yao kutokana na kutojitambua, kujiamini na kuthubutu ikwia
ni pamoja na kufanya kazi zao kwa shinikizo la usiasa badala ya kuangalia namna
ya kutumia jamii.
|
No comments:
Post a Comment