Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, July 18, 2012

RC MBEYA AWATAKA WATENDAJI WA HALMASHAURI KUFANAYA KAZI KWA UMAKINI NA UWADILIFU



Mkuu wa mkoa wa mbeya Abass Kandolo amewataka watendaji wa halmashauri ya Rungwe kuwajibika kwa kuafanya kazi kwa kuongeza umakini na  uadilifu ili kuongeza ufanisi wa kazi katika kusimamia miradi inayotekelezwa  katika Wilaya ya Rungwe.

Akiongea na madiwani na watendaji wilayani Rungwe Kandolo amewataka watendaji kuacha  suala la uzembe kazini na kuongeza uadilifu  ili wananchi wanufaike na maendeleo kuliko viongozi kuwa kikwazo cha maendeleo, pia amewataka madiwani kusimamia pesa zote za halmashauri maana ndio kazi waliotumwa na wananchi kusimamia utekelezaji wa miradi yote ya wilaya.
Zaidi Kandoro amekemea vikali tabia ya baadhi ya watu na viongozi wakihusika kuwashawishi watu kufanya vulugu kwa kisingizio cha kukomboa kutolipa kodi kwakuwa wilayani Rungwe kumeanzishwa kikundi cha Opareshen Komboa ili kuwafanya wananchi kukataa kulipa Ushuru na kutolipa michango mbalimbali ya kijamii, amesema kuwa kodi ndizo pesa za maendeleo ya wananchi hivyo inapaswa wananchi kushiriki katika masuara maendeleo kwa kulipa  kodi na michango.
Naye katibu tawala wa mkoa wa mbeya Mariam Mutunguja amewataka watendaji wa halmashauri ya Rungwe kutofanya kazi kwa mazoea kwa kutokuwa na mipango kazi ambayo inasababisha utekelezaji mmbovu wa kazi na miradi ya wananchi. zaidi amesema kuwa uwezo wa kufanya kazi upo lakini amewataka watendaji kufanya kazi ili kuifanya wilaya ya Rungwe kuwa 

mfano wa utekelezaji wa miradi.
Baada ya mjadala mrefu naye mwenyekiti wa Halmasauri ya Rungwe mheshimiwa Mwakipunga amewataka viongozi kulinda amani maana hali ya amani katika wilaya imekuwa mbaya kwani kila kukicha maandamano na migomo ya kutolipa kodi na michango ya maendeleo hii itasababisha kutotekelezwa kwa miradi ya wananchi hivyo amekemea viongozi kushiriki katika masuala ya kuvunja amani katika jamii.
Zaidi amewataka watendaji kupunguza uzembe kazin na mazoea ya kazi kwa kutimiza wajibu ili kuiletea maendeleo wilaya ya rungwe
Wilaya ya Rungwe imepata HATI safi kwa mwaka uliokwisha wa fedha hii inaonyesha usimamizi mzuri wa fedha za wananchi, na Hati safi sio kigezo cha utekelezwaji wa miradi yenye thamani na    sawa na pesa pesa iliyotumika.

Na Ally Kingo Tukuyu

No comments: